NA MWANDISHI WETU.
MWENYEKITI wa TANESCO Sports Club , Omary Shabani amesema kuwa mwaka huu TANESCO imejiandaa kuchukua makombe yote katika mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma , Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) yanayoendelea jijini Mwanza.
Mashindano ya SHIMMUTA kwa mwaka huu 2019 yanafanyika katika viwanja tofauti huku jijini humo yakihusisha jumla ya timu 46 ikiwa ni ongezeko la klabu 20 kwani ya mwaka jana yaliyo fanyika Jijini Dodoma yalikuwa na timu 26.
Akizungumzia maandalizi ya TANESCO, Shabani alisema maandalizi ya timu zote yamekamilika na mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja hivyo ndoto ni kuchukua mataji ya michezo yote inaanza kutimia taratibu.
"Mwaka Jana kule Jijini Dodoma tulikuwa mabingwa wa jumla, pia msimu huu tunataka kufanya hivyo na kuongeza vikombe zaidi katika michezo yote ambayo tunashiriki, maandalizi yalifanyika mazuri , hatuna shaka tutafanya hivyo" alisema Shaban.
Kwa upande wake Meneja wa TANESCO katika mchezo wa Netball, Nazareth Mwanjala alisema mashindano hayo ni muhimu kushiriki kwani husaidia kuleta maendeleo pia hupelekea kufahamiana miungoni mwa Washiriki hivyo hubadilisha mawazo na uzoefu wa kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: