MEYA wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Jafari, anatarajia kufanya hafla ya kuwafariji jumla ya Watoto Yatima na Wajane 6,000 Desemba 31 mwaka huu katika Ukumbi wa PTA uliopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili, mratibu wa hafla hiyo, ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya kusaidia Wajane na Watoto Yatimba ijulikanayo kama TFTF, Juma Mark, alisema kuwa maandalizi ya shughuli hiyo maalumu yamekamilika ambapo kutakuwa na huduma ya Chai, Chakula cha mchana na usiku.
Aidha alisema kuwa hafla hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Meya Temeke kwa ushirikiano na Taasisi ya kusaidia Wajane na Watoto Yatimba TFTF.
“Hafla hii imeandalia na Ofisi ya Meya wa Temeke kwa ushirikiano na Taasisi ya kusaidia Wajane na Yatima TFTF, ambapo tunatarajia kuwa na jumla ya Watoto Yatima na Wajane 6,000 ambao tumewaandalia kuanzia Chai ya asubuhi, Chakula cha mchana na cha usiku pamoja na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya’’. Alisema Juma.
Juma aliweka wazi kuwa katika hafla hiyo pia kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya pamoja na ngoma za asili.
Katika kusherehekea siku hiyo maalumu Meya wa Temeke akishirikiana na Taasisi ya TFTF wanatarajia kutembelea wagonjwa katika Hospitali za Temeke na Mbaga na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa kwa wiki nzima kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku hiyo maalumu.
Aidha Juma aliwataka Wajane na Yatima mbalimbali kujitokeza siku hiyo katika Ukumbi wa PTA ili kufurahi kwa pamoja na baadhi ya viongozi watakaotajwa hapo baadaye ikiwa ni pamoja na kupata burudani mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: