Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda akiongea na wadau wa elimu mkoani Iringa wakati tathimini na utangazwaji wa matokeo ya darasa la saba
Baadhi ya wadau wa elimu walioshiriki kikao hicho
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda amewataka wananchi kuwa walinzi wa watoto wa kike ili kumaliza tatizo la mimba za utotoni ambazo zimekuwa zinakatisha ndoto za watoto.
Kauli hiyo ameitoa wakati akitangaza matokeo ya darasa la saba ya mkoani katika msimu wa mwaka huu wa 2019, Seneda amesemakuwa kila wananchi anapaswa kuwa mlinzi wa kila mtoto ili afanikiwe kutimiza ndoto zao.
“Kila mmoja awe mlinzi wa mtoto kwa kuwa hawa wanaowapatia mimba watoto wa kike nao wanawatoto hivyo tukiwalinda watoto hao watatimiza ndoto zao na kuleta faida kwa taifa letu” alisema Seneda
Seneda alisema kuwa zambi ya kuwapa mimba watoto wa kike haiwezi kuisha kwa kuwa ukifanya hivyo basi hata mtoto wako atakuja kufanyiwa hivyo kwa kuwa malipo yapo hapa hapa duniani.
“Tunawajibu wa kuhakikisha tunaendelea kutoa kutoa elimu shuleni ili kutokomeza kabisa tatizo hilo kwa kubadilishani mawazo na watoto wa kike kwa lengo la kujua tatizo nini ambalo linasababisha mimba za utotoni” alisema Seneda
Aidha Seneda alisema kuwa watoto wengi wa kike wanashindwa kuendelea kutokana na kuwa na mimba ya utotoni hivyo ni lazima wazazi na walezi kuwalinda watoto.
“Watoto wengi wanakatishwa ndoto zo licha ya kuwa wengi wamekuwa wanaakili ambazo zingekuwa msaada kwa maendeleo yake binafsi na taifa kwa ujumla hivyo wazazi na walezi wanawajibu wa kuwafundisha tabia nzuri ili nao wajirindi na mimba za utotoni” alisema Seneda
Nao baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho wamesema kuwa kuna haja ya kubaridishwa kwa sheria hiyo ili kuwabana wanaume wanaofanya vitendo hivyo kwa watoto wa kike.
Toa Maoni Yako:
0 comments: