Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akitoa nenowakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wenyeviti wa serikali, wajumbe wa mitaa pamoja na watendaji kata iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomi Ostarbey.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Harodi Maruma akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wenyeviti wa serikali, wajumbe wa mitaa pamoja na watendaji kata iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomi Ostarbey.
Wajumbe wakifuatilia mafunzo yaliokuwa yakitolewa katika ukumbi wa king Solomon leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amesema kuwa ameanzisha kampeni ya utoaji tuzo kwa mitaa itakayofanya vizuri kwenye suala la usafi ambapo kila mtaa utapatiwa zawadi ya fedha tathilimi.
Aidha Chongolo amewaonya wananchi wanaotupa taka hovyo na hivyo kuwataka watendaji hao kusimamia sheria kwa watakaojihusisha na uharibifu huo wa mazingira ikiwemo kulipa faini kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Chongolo ametoa kauli hiyo leo, wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wenyeviti wa serikali, wajumbe wa mitaa pamoja na watendaji kata iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomi Ostarbey.
Mhe. Chongolo amesema kuwa lengo la kampeni hiyo, ni kuongeza motisha katika kuboresha Halmashauri hiyo kuwa katika muonekano mzuri, na kuwasisitiza watendaji hao pamoja na wenyeviti wa mitaa kusimamia kwa ukamilifu.
Amefafanua kuwa tuzo hiyo itatolewa kila maada ya miezi mitatu ambapo mtaa utakaoibuka na ushindi itapatiwa fedha tathilimu kiasi cha shilingi 500, 0000, mshindi wa pili 300,000 huku mshindi wa tatu akipata shilingi 200,000.
“Halmashauri ya Kinondoni ni safi, lakini tunatakiwa kufanya vizuri zaidi , kwa mantiki hiyo tunakuja na kapmeni ya usafi wa kila mtaa, watakaofanya vizuri watapatiwa zawadi ya fedha, na fedha hizo zitabaki kwenye mitaa yenu kwa ajili ya shuguli nyingine” amesema Mhe. Chongolo.
”Watakaoendesha mchakato huo ni nyie wenyeviti na wajumbe wa mitaa, kazi yangu mimi ni kuweka fedha kwa ajili ya kutoa zawadi, na kampeni hiyo tunaianza leo hii arehe nne mwezi wa 12 kwa hiyo ikifika tarehe nne mwezi watatu 2020 tutatoa tuzo hiyo kwa mitaa itakayokuwa imeshinda.
Aidha Mhe. Chongolo ameongeza kuwa pamoja na tuzo hizo kutolewa amewataka watendaji kusimamia sheria na kanuni za utunzaji mazingira ikiwemo kutoza faini kwa watu wanaotupa taka hovyo kwani kwakufanya hivyo wataongeza ufanisi na ubora wa mitaa kuendelea kuwa misafi.
“Zipo sheria za usafi ambazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria lakini hazifuatwi, watendaji, wenyeviti na wajumbe mliopo hapa nendeni mkazisimamie vizuri”amesisitiza.
Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amewataka viongozi hao kusimamia mapato vizuri sambamba na kuepuka rushwa kwa kuwa kufanya hivyo kutawaingiza kwenye matatizo makubwa.
“ Kunasuala la rushwa, ni waonye msijihusishe na mambo hayo, leo hii hapa kuna maafisa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wapo hapa nawao wata waeleza madhara ya kupokea au kutoa rushwa, niwaombe sana msikilize kwa makini na mkayafanyie kazi” ameongeza Mhe. Chongolo.
Kwa upande wake Afisa utumishi mkuu wa Halmashauri hiyo Bi Faudhia Nombo amesema kuwa lengo la mafunzo hayo elekezi ni kuwawezesha viongozi hao ili waweze kutekeleza majukumu ya usimamizi na undeshaji wa shughuli mbalimbali katika mitaa yao kwa kuzingatia Sera, Sheria , Taratibu ,Kanuni na miongozo iliyopo ilikuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: