Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo, akizungumza na wakurugenzi wa mamlaka za maji na watendaji wakuu wa sekta hiyo wakati akifungua mkutano wa uendeshaji wa kisekta mjini Singida leo.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Barnabas Ndunguru, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Ewura, Lawrence Sawe na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maji, Adam Karia. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Anthony Sanga (kushoto),akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo baada ya kufungua mkutano huo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano huo.
Watendaji wakuu wa Sekta ya Maji nchini wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Watendaji wakuu wa Sekta ya Maji nchini wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea

Na Dotto Mwaibale, Singida.

KATIBU Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amewataka watendaji wa mamlaka za maji nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawe wabunifu ili kukuza mapato ya sekta hiyo.

Ameyasema hayo alipokutana na wakurugenzi wa mamlaka za maji na watendaji wakuu wa sekta hiyo wakati akifungua mkutano wa uendeshaji wa kisekta mjini Singida leo. 

" Zamani mamlaka za maji zilikuwa zikitoa huduma lakini sasa hivi zinaendelea kutoa huduma na pia ujenzi wa miradi ya maji haya ni mabadiliko makubwa sana kisekta hivyo zingatieni ubunifu katika utendaji wenu" alisema Mkumbo.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo kuna kila sababu ya kupitia muundo mpya wa utumishi kuanzia ngazi ya wizara na taasisi ili kuiweka katika mifumo inayoeleweka.

Amesema kupitia mfumo huo mpya itasaidia taasisi husika kuweza kuchagua wahandisi wenye viwango stahiki kukidhi matarajio ya miradi kwa ufanisi.

"Tunakusudia kuanza kuzingatia vigezo ikiwemo kuangalia ni mradi gani apewe mkandarasi kulingana na sifa na uwezo alionao kuweza kusimamia mradi husika" alisema.

Mkumbo amesisitiza kuwa yote hayo yatawezekana kama kutakuwepo na ushirikiano wa dhati baina wa watendaji wa sekta ya maji na wadau wote kwa ujumla.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: