Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza katika mkutano wa mkutano wa Mawaziri sekta za Mazingira, Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa Jangwa la Sahara SADC (SADC) uliofanyika jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri sekta za Mazingira,Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara SADC (SADC) uliofanyika jijini Arusha.
Mawaziri wanaosimamia sekta za Mazingira, Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC), wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wanaosimamia sekta za Mazingira, Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara (SADC).

Na Vero Ignatus, Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu amefungua mkutano wa Mawaziri wanaosimamia sekta za Mazingira, Utalii na Maliasili kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) uliofanyika jijini Arusha.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Mhe,Samia Suluhu ameeleza kusikitishwa na uharibifu wa mazingira katika nchi wanachama wa jumuiya Ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).

Amesema anaimani mkutano huu utaweka mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kuzuia kuingia kwa viumbe vamizi,ambapo viumbe hivyo vinaweza kuhatarisha ustawi wa sekta za kilimo, uvuvi, mifugo na utalii pamoja na hifadhi ya bioanuia

''Nafahamu kuwa kunajuhudi mbalimbali za kudhibiti viumbe vamizi nikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mpango mkakati na mpango kazi kudhibiti viumbe hivi"Alisema Mhe.Samia.Amesema ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira ni muhimu kuwa na mikakati ya pamoja ya uhifadhi wa mazingira ili kukabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema kuwa Sekta ya utalii imekuwa na mchango mkubwa katika nchi za SADC kwani inachangia dola 56.3 bilioni sawa na asilimia 8.2 ya pato ghafi,ambapo imechangia ajira ya watu 6.3 milioni, ambapo mwaka 2018 sekta hiyo ilichangia dola bilioni 2.4 sawa na asilimia 25 fedha za kigeni.

Amezitaka nchi wananchama kuweka mikakati na kuridhia itifaki ya mazingira ili kutunza mazingira na kuweka jitihada za pamoja za kuhifadhi mazingira ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

“Kazi ya Kuhifadhi na kulinda mazingira yetu ni yetu Wenyewe “Anaeleza Makamu wa Raisi akifafanua umuhimu wa kutunza mazingira. Makamu wa Raisi amesema kuwa serikali zinasubiri mapendekezo yanayotokana na mkutano huo kwa ajili ya utekelezaji kwa maslahi mapana ya SADC na nchi wanachama.

Aidha amesema kuwa ili kuweza kuwa na utalii endelevu ni lazima kuhifadhi mifumo ya ikolojia ya misitu wanyamapori, viumbe vya majini, fukwe, mabonde ya asili,kutokana na ukweli kuwa rasilimali mbalimbali zilizopo za kimazingira,maliasili na utalii, hazitambui mipaka ya kijiografia. 

Waziri waMaliasili na Utalii, Dk Hamis Kingwangala amesema majukumu ya mkutano wa leo ni kuridhia mapendekezo mbalimbali ya kulinda maslahi ya nchi wanachama, ambapo wanatarajia kuangalia changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

"Pia tutajadili utekelezaji itifaki ya kuwalida wanyamapori nausimamizi na utunzwaji wa misitu" amesema Kigwangala. Mhe. Kigwangala amesema kuwa Mawiziri hao watapitisha mapendekezo ya kuwa na mkakati wa pamoja wa kupambana na ujangili na kuhakikisha kunakua na utalii endelevu.

Pia tutaangalia itifaki ya SADC Kuhusu usimamizi wa misitu, itifaki ya mpango wa maendeleo ya utalii kwa nchi zote. Wanachama wa SADC ni nchi 16 ambazo ni Angola, Botswana, Comoros, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: