Mvua zinazoendelea kunyesha mkoa wa Tanga zimezidi kuleta maafa, baada ya usiku wa kuamkia leo Oktoba 26, 2019 kukata barabara kati ya Handeni na Korogwe katikati ya kijiji cha Misima na Sindeni. Pichani ni gari la abiria aina ya Noah likiwa limetumbukia mtoni. Noah hiyo inayodaiwa ni ya abiria, na ilikuwa inatoka Handeni kwenda Korogwe, ilipofika hapo alfajiri ya leo, dereva hakujua kuwa barabara imekatika, hivyo akajikuta anaingia kwenye mto. Inadaiwa watu kadhaa wamepoteza maisha.
Home
AJALI
HABARI
HABARI NA MATUKIO
HABARI ZA KIJAMII
BARABARA YA HANDENI NA KOROGWE ENEO LA KIJIJI CHA MISIMA NA SINDENI HALI TETE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments: