Naibu Spika Mhe. Tulia Akson akipeana mkono na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Mhe. Aisharose Matembe baada ya kukabidhi gari la wagonjwa lenye thamani ya sh.milioni 21 na vitanda 16 vya wagonjwa, viwili vikiwa vya kujifungulia wajawazito vilivyotolewa na mbunge huyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida katika hafla iliyofanyika viwanja vya hospitali hiyo mjini Singida jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Hassan Kilimba na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dk.Rehema Nchimbi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Hassan Kilimba akizungumza katika hafla hiyo.
Naibu Spika Tulia Akson akimtuza Msanii Musa Saidi (maarufu Musa Mashairi)
Wanawake wakipiga makofi katika hafla hiyo.
.Wanawake wakipiga makofi katika hafla hiyo.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Deogratius Manuba akisoma taarifa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Mshereheshaji wa hafla hiyo, Salma Mwijuma akiwajibika.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aisharose Matembe akizungumzia msaada huo.
Mhe.Tulia Akson akiserebuka pamoja na viongozi mbalimbali katika shughuli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi akizungunza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Hassan Kilimba akiteta jambo na Naibu Spika Tulia Akson.
Mhe.Tulia Akson akikabidhiwa kibuyu wakati akipewa heshima ya kusimikwa kuwa shujaa wa kabila la Kinyaturu na kupewa jina la Liti ambalo lilikuwa ni la shujaa wa kabila la Wanyaturu aliyeshindana na wakoloni.
Mhe.Tulia akiwa amekibeba kibuyu alichokabidhiwa.
Mhe.Tulia akihutubia.
Mapokezi ya gari la wagonjwa yakifanyika.
Mhe.Tulia akimkabidhi kitanda Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini Mhe. Elia Digha.
Mhe.Tulia akimkabidhi kitanda Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini, Lucas Kazingo.
Mhe.Tulia akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Singida.
Mhe.Tulia Akson akifurahi na wakina mama baada ya kukabidhi vifaa hivyo.
Mkazi wa Singida, Mwanahamisi Jumanne akielezea kufurahishwa kwake baada ya kutolewa kwa msaada huo na mbunge huyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
NAIBU Spika Tulia Akson amekabidhi gari la wagonjwa lenye thamani ya sh.milioni 21pamoja na vitanda 16 viwili vikiwa ni vya kujifungulia wajawazito katika hafla iliyofanyika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa.
Gari hilo la wagonjwa na vifaa tiba hivyo vimetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aisharose Matenbe kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dkt.John Magufuli katika sekta ya afya mkoani humo.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika juzi katika viwanja vya hospitali hiyo, Tulia alisema Mbunge huyo anatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa dhati ya moyo wake.
"Nikiwa kama kiongozi wa wabunge nawafahamu wabunge wote na kazi za maendeleo wanazozifanya katika majimbo yao hivyo ni seme kiukweli Aisharose Matembe anafanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa wa Singida tena anatoa na fedha zake binafsi hivyo anapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo wa mkoa wenu" alisema
Tulia.
Matembe akizungumzia msaada huo alisema amekuwa akiumia sana pale anapokuwa katika ziara zake za kikazi kuwatembelea wananchi na kukutana na changamoto zao mbalimbali zikiwemo za mazingira bora ya kujifungulia wakina mama na vitanda vya kulalia wagonjwa ndio maana akaguswa na kuamua kutoa fedha zake na kununua gari hilo la wagonjwa na vitanda kwa ajili
ya kusaidia wananchi.
"Nimekuwa nikifanya ziara za kikazi mkoa mzima na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa msaada wa serikali na wakati mwingine kwa kutumia fedha zangu" alisema
Matembe.
Alisema kitanda kimoja cha kujifungua kitapelekwa katika Zahanati ya Kijiji cha Tumuli Mkalama na kingine kitapelekwa Zahanati ya Mughunga ambayo ina hudumia vijiji vitano.
Alitaja zahanati zingine zilizopata vitanda hivyo kuwa ni Ighombwe kitanda kimoja,, Kinyeto kitanda kimoja, Rungwa vitanda vitatu , Kituo cha Afya Sokoine vitanda vitano na Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida vitanda viwili.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Juma Kilimba alisema kwa miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano vituo vya afya 11 vimejengwa na Hospitali mbili za Wilaya za
Ilongero na Mkalama na maboresho ya Hospitali ya Sokoine na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mandewa.
Alitaja miradi mingine iliyofanywa na serikali kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, umeme, maji na kilimo.
Mkuu wa mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbi alisema anaomba ile dhana ya kuwa mkoa wa Singida ni maskini iondolewe kwani mkoa huo upo vizuri ndio unaoongoza kwa kutoa kuku walio bora, ndio ulio na kiwanda kikubwa cha mafuta ya alizeti Afrika Mashariki na Kati, uzalishaji wa asali, kilimo cha vitunguu na viazi vitamu na kuchangia maji kwenda kwenye mradi mkubwa wa umeme Rufiji.
Mkazi wa Singida Mwanahamisi Jumanne alimshukuru mbunge huyo kwa jitihada zake za kutatua changamoto za wananchi hasa kwa wanawake kwa kuwanunulia vitanda hivyo vya kujifungulia
na kusaidia vikundi vyao vya ujasiriamali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: