Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (mwenye miwani walioshika bendera) akikabidhiwa bendera ya Taifa baada ya kuzungumza na waandishi wa habari za michezo wanao kwenda nchini Burundi kuiunga mkono timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) 
 Kingu akisalimiana na waandishi wakati alipowapokea Manyoni mkoani Singida leo hii asubuhi.
 Kingu akisalimiana na waandishi wakati alipowapokea Manyoni mkoani Singida leo hii asubuhi.
 Mbunge Kingu akiwaelekeza jambo waandishi hao.
 Waandishi wa habari wakimuhoji Mbunge Kingu.
Mtangazaji wa habari za michezo wa Kituo cha EATV na East Africa Redio, Zainabu Rajabu (kushoto) na Mchambuzi wa Michezo wa Kituo hicho, Tigana Lukinya wakimkabidhi fulana 
Mbunge Kingu.

Na Dotto Mwaibale, Manyoni

MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, ameupokea msafara wa Waandishi  wa habari za michezo  wanaokwenda nchini Burundi kwa ajili ya kuiunga mkono Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' inayokwenda kucheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali  Kombe la Dunia zitakazofanyika  nchini  Burundi.

Akizungumza wakati akiupokea msafara huo wa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali zaidi ya 30 kutoka Dar es Salaam wilayani Manyoni mkoani Singida alipo waandalia kifungua kinywa  kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Burundi,  Kingu alisema  amefurahishwa na uzalendo mkubwa wa waandishi hao kwa kuamua kwenda Burundi kuipa sapoti timu ya taifa katika mchezo huo muhimu wa kuwania kufuzu. 

"Nawapongeza kwa uzalendo huu ambao mnaufanya, kiukweli siyo jambo dogo, nipo huku kwa ajili ya ziara za kijimbo ambazo huwa nafanya siku za wikiendi lakini niliposikia mnapita nikasema nitawaona, nimefurahi na hakika mnakwenda kuwa sehemu ya historia ya nchi,"  alisema Kingu

Alisema uzalendo huo waliouonesha ni wa mfano na utawaongezea ari wachezaji wetu na kuhakikisha timu yetu inapata ushindi mkubwa.

Kabla ya kuanza kwa safari hiyo baada ya kupata kifungua kinyea hicho wanahabari hao walimshukuru Kingu ambapo  walimfanyia dua na kumuahidi kuwa watakwenda kuwa mabalozi wazuri nchini Burundi kwenye mchezo huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: