Mkurugenzi wa Idara ya wateja wa kati na wadogo wa Benki ya NBC, Bw Elibariki Masuke (katikati) akifafanua jambo wakati wa wa uzinduzi wa kampeni ya huduma mpya ya kidijitali ya benki hiyo iliyopewa jina ‘Kulipa Inalipa’ iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kidigitali kutoka benki hiyo Bw Deogratius Mosha (Kushoto) na Mkuu wa Tawi la Kati la benki hiyo Bi Maraiam Kombo (kulia).
Mkuu wa Idara ya Huduma za Kidigitali kutoka benki hiyo Bw Deogratius Mosha (Kushoto) akifafanua jambo wakati wa wa uzinduzi wa kampeni ya huduma mpya ya kidijitali ya benki hiyo iliyopewa jina ‘Kulipa Inalipa’ iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wa kati na wadogo wa Benki ya NBC, Bw Elibariki Masuke (katikati) na Mkuu wa Tawi la Kati la benki hiyo Bi Maraiam Kombo (kulia).
Mkuu wa Tawi la Kati la benki hiyo Bi Maraiam Kombo (kulia) akifuatilia huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa mmoja wa wateja waliofika kwenye tawi la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya huduma ya mpya ya kidijitali ya benki hiyo iliyopewa jina ‘Kulipa Inalipa’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC Bw Oswald Kashasha (Kulia) akiendesha zoezi la usajili wa Kidijitali kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa kampeni ya huduma ya mpya ya kidijitali ya benki hiyo iliyopewa jina ‘Kulipa Inalipa’ iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Tawi la Kati la benki hiyo Bi Maraiam Kombo (kushoto)

Benki ya NBC leo imezindua huduma yake maalumu ya kidijitali ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kurahisisha huduma ya malipo kwa wateja wake wanaofanya miamala ya malipo kwa taasisi mbalimbali ikiwemo malipo ya serikali, umeme na huduma za maji.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya wateja wa kati na wadogo wa Benki ya NBC, Bw Elibariki Masuke alisema huduma inayohusisha usajili wa chini ya muda wa dakika tano tu na inaondoa kabisa matumizi ya karatasi katika usajili ambao hapo awali ulikuwa ukitumia muda mrefu huku pia ukihusisha mahitaji ya nyaraka nyingi.

“Kupitia huduma hii mteja anachotakiwa ni kufika tu kwenye matawi yetu akiwa na kitambulisho cha uraia kutoka NIDA na ndani ya dakika 5 tu tayari atakuwa amefanikiwa kujisajili sambamba na kupatiwa kadi yake ya ATM na kuunganishwa na huduma ya Simbanking,’’.

“Na kwa wateja ambao watashindwa kufika kwenye matawi yetu wanaweza kuwatumia mawakala wetu pamoja na mamia ya maofisa wetu watakao kuwa tayari kuwasaidia kufanikisha usajili huo bila gharama yoyote,’’ alibainisha.

Kwa mujibu wa Bw Masuke huduma hiyo ya Kidijitali itawasaidia wateja wanaolipa ankara za maji, ankara za huduma za televisheni na huduma ya kutuma fedha bila kuhitaji kubeba fedha.

Alisema kampeni hiyo inafahamika kama ‘Kulipa Inalipa’ ikimaanisha kwamba mteja wa benki hiyo atanufaika kwa kufanya malipo kupitia huduma hiyo na kwamba mteja anapojisajili kupitia huduma hiyo ataingia moja kwa moja kwenye droo ambayo kila siku itatoa zawadi ya fedha kiasi kisichopungua sh 10,000 kwa mshindi.

Aliongeza kuwa kupitia huduma hiyo wateja wa benki hiyo wanaepushwa na gharama za kutoa miamala kwenye mashine za kutolea fedha za ATM pamoja na huduma ya mwezi ya kuhudumia akaunti zao isipokuwa watatozwa gharama pale tu watakapotumia huduma za dirishani (teller).

“ Shukrani zetu za dhati kabisa ziende kwa Serikali yetu kwa kuhamasisha matumizi ya vitambulisho vya Uraia kwa kila mwamanchi na hivyo basi kupitia vitambulisho hivyo usajili wa kidigitali unahusishwa na vitambulisho hivyo na hivyo kuwahakikishia wateja wetu usalama wa fedha zao kwenye akaunti,’’ aliongeza.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Huduma za Kidigitali kutoka benki hiyo Bw Deogratius Mosha alitoa wito kwa jamii kufungua akaunti na benki hiyo kwakuwa imefanya mabadiliko makubwa kwa kuwekeza kwenye huduma za huduma za kisasa yakilenga kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja wa benki hiyo.

Akizungumza wakati akijisajili kupitia huduma mteja Bi. Merinda Marando aliipongeza benki hiyo kwa kurahisisha huduma hiyo ambayo kabla ilikuwa ikitumia muda mrefu huku pia ikihusisha mlolongo mrefu wa mahitaji ya taarifa za kujaza kabla ya kujisajili na huduma za kibenki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: