Mkurugenzi wa Biashara na Wateja wadogo na wakati wa benki BancABC Joyce Malai akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kuzindua akaunti ya IZZE ya benki hiyo. Benki ya BancABC imezindua akaunti mpya ya IZZE ambayo ni rahisi kufungua na haina makato yeyote ya mwezi na mteja atapata riba hata akiwa na kianzio cha shilingi Elfu Kumi (Tshs10, 000/-)
 Meneja wa Huduma za Uwakala BancABC Mwita Rhobi akiongea jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua akaunti mpya ya IZZE. Benki ya BancABC imezindua akaunti mpya ya IZZE ambayo ni rahisi kufungua na haina makato yeyote ya mwezi na mteja atapata riba hata akiwa na kianzio cha shilingi Elfu Kumi (Tshs10, 000/-)
Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi akionyesha bango baada ya kuzindua akaunti mpya ya IZZE leo jijini Dar es Salaam. Benki ya BancABC imezindua akaunti mpya ya IZZE ambayo ni rahisi kufungua na haina makato yeyote ya mwezi na mteja atapata riba hata akiwa na kianzio cha shilingi Elfu Kumi (Tshs10, 000/-). Wengine ni Mkurugenzi wa Biashara na Wateja wadogo na wakati wa benki BancABC Joyce Malai (kati kati) na Meneja wa Huduma za Uwakala BancABC Mwita Rhobi (kushoto).

Benki ya BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara leo imeendelea kudhihirisha ubunifu wake katika huduma zinazowanufaisha wateja wake baada ya kutangaza kuzindua akaunti mpya ya IZZE ambayo ni rahisi kufungua na haina makato yeyote ya mwezi.

Kupitia akaunti ya IZZE ya BancABC, mteja anahitaji kuwa na kitambulisho cha taifa tu kilichotolewa na NIDA ili kufungua akaunti hiyo, na atapata riba hata akiwa na kianzio cha shilingi Elfu Kumi (Tshs. 10,000/-)

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua akaunti hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Wateja wadogo na wa kati wa benki BancABC Joyce Malai alisema, ‘Leo kwenye soko la biashara watu wengi wanaangalia sehemu watakayo nufaika kuwekeza fedha zao na yenye uhakika wa kupata faida/manufaa kadhaa. Uhakika wa kupata faida au manufaa ni moja ya malengo muhimu kwa kila mtanzania. 

Vile vile, kufungua akaunti ya benki kwa siku hizi imekuwa ikichukuliwa kama hatua ngumu yenye kuhitaji muda na zaidi inaonekana kama inalenga watu wenye kipato kikubwa. Sisi BancABC tumelifanyia kazi suala hilo na ndio sababu tumekuja na akaunti ya IZZE ambayo ni rahisi kufungua kwani mteja anaweza kufungua akaunti hii hata kupitia mawakala wetu popote nchini’, Malai alisema.

Malai aliongeza kuwa akaunti ya IZZE ni Rahisi kufungua kama ilivyo jina lake. Mteja anahitajika kuwa na kitambulisho cha taifa TU na haina kiasi chochote cha kuanzia, haina makato ya mwezi na muhimu zaidi ni kwamba mteja anapata riba kila mwezi ikiwa ana salio kuanzia shilingi elfu kumi (Tshs. 10,000/-) au zaidi kwenye akaunti yake.

Akaunti hii imeunganishwa kwenye mtandao wetu wa BancABC Mobi kupitia USSD (*150*34#) na Aplikesheni yetu kwa hivyo mteja haitaji kila mara kutembelea matawi yetu kwa ajili ya kuweka au kutoa hela. Vile vile mteja anaweza kutumia akaunti yake kupitia machine za ATM zenye nembo ya Visa, mawakala wa BancABC pamoja na “internet banking” Mteja wa IZZE akaunti atapata huduma hizi zote za kibenki kwa masaa 24 siku saba za wiki popote alipo. Zaidi, mteja atakuwa akipata ujumbe mfupi bure kupitia simu ya kikanjani yaani sms kila mara anapofanya muamala wa kuweka ama kutoa pesa na kupata huduma ya mikopo baada ya hapo.

Kwa upande wake, Meneja wa huduma za uwakala wa benki hiyo Ndugu, Mwita Rhobi alisema kuwa BancABC imewawezesha mawakala ambao wanapatikana nchini kote kusaidia zoezi la ufunguaji wa akaunti ya IZZE. Mawakala hawa wataweza kufanya hatua zote za kufungua akaunti kidigitali na mtu yeyote anayehitaji kufungua akaunti ya IZZE atafanikisha huduma hiyo kwa muda usiozidi dakika tano na papo hapo mteja anaanza kuweka pesa kwenye akaunti yake kupitia aidha mawakala wetu wa BancABC, matawi yetu ama kupitia kuhamisha fedha kutoka kwenye mitandao ya simu kwenda kwenye akaunti yake aliyoifungua kirahisi kabisa.

Uboreshaji wa huduma kama hii ni moja kati ya juhudi za BancABC kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ili kusaidia ukuaji wa huduma jumuishi za kifedha kwa kila Mwananchi pamoja na wateja wetu popote walipo. Kupitia akaunti ya IZZE Mtanzania yeyote anayefungua akaunti hii ataweza kupata riba hata akiwa na kianzio cha shilingi elfu kumi tu, Rhobi aliongeza.

“Hivyo basi, natoa rai kwa kila Mtanzania mwenye kitambulisho cha Taifa (NIDA) kutembelea tawi lolote la BancABC au mawakala wetu kufungua akaunti ya IZZE kwa urahisi kabisa na kupata manufaa kedekede kama mlivyosikia hapo awali, Rhobi alisisitiza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: