Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (TPDC), Dkt. James Matarajio, akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo, wakati wa maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC katika Viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, leo kuelekea Mkutano Mkuu wa Nchi Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika utakaoshirikisha jumla ya Nnchi 16 za Jumuiya hiyo unaoanza Agosti 9 kwa Mawaziri na kwa Marais utafanyika kwa siku mbili.
 Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu akiongea na mwananchi aliyetembelea banda lao kujua huduma zao.
 Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu akiongea na wanahabari.
Mfanyakazi wa TPDC (kulia) akizungumza na mwananchi aliyetembelea banda lao kujua huduma wanazotoa.

Wafanyakazi wa TPDC wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limejipanga kuendelea kutoa huduma zilizo bora kwa wateja wake ili kuwapunguzia matumizi ya fedha.

Hayo yamesema na Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu wakati akizungumza na wanahabari waliofika kujionea huduma wanazotoa katika maonesho ya 4 wiki ya Viwanda kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Bi. Msellemu amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kufungua vituo vingi zaidi kwa ajili ya kusambaza gesi asilia inatumika katika magari ikiwa na kuongeza zaidi upatikanaji wa gesi hiyo majumbani.

"Tupo katika mkakati wa kufungua vituo vingi zaidi vya kujazia gasi kwa wale wateja wetu wanaotumia gesi katika magari na pia tunawashauri Watanzania kununua magari yanayotumia gesi ili kuweza kupunguza matumizi," amesema.

Amesema kuwa mpaka sasa zoezi la kuwaunganishia gesi majumbani linaendelea vyema na wamefikia nyumba zipatazo 1000 toka kwa vile nyumba 70 walizoanza nazo awali katika mkoa ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa mkakati wao mwingine ni Kuchimba gesi yao wenyewe Mnazi Bay Kaskazini na Songosongo Magharibi ... ikiwa na kauli mbiu ya kufanya mazingira wezeshi

Mpaka sasa wamejipanga zaidi kuweza kusambaza gesi katika nchi wanachama wa SADC japo kwa sasa nchi za Kenya, Uganda na Zambia zimeonyesha nia ya kutaka kusambaziwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: