Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye (wa pili kutoka kushoto) akiambatana na Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt.Hassan Abbasi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA-Zambia, Mhandisi.Bruno Chingandu (wa kwanza kulia) na Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah wa pili kulia wakiwa katika uzinduzi wa mitambo ya kunyanyulia mizigo stesheni ya Fuga.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akivaa kofia kujiandaa kuwasha moja ya mitambo ya kunyanyulia mizigo ya ujenzi wa mradi wa Umeme JN HPP iliyopo katika Stesheni ya Fuga, wa kwanza kushoto ni Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akiendesha  moja ya mitambo ya Kunyanyulia mizigo iliyoko katika stesheni ya Fuga wakati wa ufunguzi wa mitambo hiyo hapo jana Agosti 19, 2019.
 Wafanyakazi wa Stesheni ya Fuga wakishuhudia uwezo wa mtambo aina ya Raech Stacker wa kunyanyua mizigo mizito katika stesheni ya Fuga uliozinduliwa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akitelemka kutoka kwenye moja ya mtambo wa kunyanyulia mizigo mara maada ya kuuzindua hapo jana katika Stesheni ya Fuga itayotumika kopokea na kusafirisha mizigo kwenda mradi wa Umeme JN HPP.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akipata maelezo fulani kutoka kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi wakati wa uzinduzi wa mitambo ya kunyanyulia mizigo ya ujenzi wa mradi wa umeme JN HPP uliofanyika katika Stesheni ya Fuga.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akipata maelezo fulani kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya usambazazi mitambo ya kunyanyulia mizigo ya Eristic (t) Investment Company, Hassan Kipussi katika uzinduzi wa mitambo hiyo uliofanyika katika Stesheni ya Fuga jana Agosti 19, 2019. (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: