Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akizungumza katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga wakati akizindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye pia Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa (katikati) na Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James wakati akizindua Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya kijani.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa, Kheri James akiimba pamoja na Msanii Beka Boy (kulia) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Wanachama wa CCM wakicheza na kupiga picha wakati wasanii Papii Kocha na Beka Boy wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Wasanii Papii Kocha na Beka Boy wakitoa burudani.
Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James akiimba wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Diwani kutoka Nzega, ambaye pia ni Msanii wa nyimbo za Asili, Madebe Jinasa (katikati) akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shinyanga ya Kijani.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM taifa),Kheri James amezindua rasmi Kampeni ya ‘Shinyanga ya Kijani’,mkakati unaolenga kuwaandaa vijana wa CCM kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nchini utakaofanyika mwishoni mwaka 2019. 

Kampeni hiyo kabambe imezinduliwa leo Jumatano,Juni 19,2019 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga. 

Akizindua Kampeni hiyo,Mwenyekiti wa UVCCM taifa,Kheri James amesema Operesheni ya Kimkakati inayojulikana kwa jina la Mkakati wa kijani kwa upande wa mkoa wa Shinyanga itakuwa ni ‘Shinyanga ya Kijani. 

“Huu ni mkakati wa kuwaandaa vijana wanachama wa CCM kote nchini kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nchini,kwa hiyo vijana wote wanaandaliwa kwa maana ya kuwaarifu kwamba mwaka huu uchaguzi utakuwepo”,alisema. 

Alieleza kuwa mkakati huo unalenga kuwataarifu kuwa vijana wanalo jukumu la kujiandikisha katika madaftari ya wapiga kura kwenye maeneo yao na kujitokeza kugombea na kuwapigia kura wale watakaogombea pamoja na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki na sheria za uchaguzi zinazingatiwa ili uchaguzi wetu uwe ni wa amani. 

“Leo nimepata heshima ya kuzindua mkakati huu katika mkoa wa Shinyanga, imani yangu ni kwamba vijana leo tunawatangazieni kwamba uchaguzi mwaka huu upo,lakini nyinyi kama wananchi wengine mnayo fursa ya kugombea sawa na wengine,ili mpate haki hiyo lazima mjiandikishe ili mpate uhalali wa kuwa wananchi wakazi kwenye maeneo utakapofanyika uchaguzi”,alifafanua. 

“Vijana mnalo jukumu la kushirikiana na chama chetu kuhakikisha wagombea wa chama chetu wanashinda uchaguzi wa serikali za mitaa,hiyo ni kazi ambayo tumekuja kuambizana leo na kuizindua rasmi katika mkoa wetu wa Shinyanga”,aliongeza James. 

Aidha aliwataka vijana walioaminiwa na kupewa nafasi za uongozi watambue kuwa kuwa wameaminiwa kwa maslahi ya umma hivyo watumike kwa maslahi ya umma huku akiwataka vijana wanaopewa madaraka na kujifanya siagi na kuyeyuka zama zao zinahesabika akidai hakuna cheo kinachodumu. 

“Tunahitaji kuwa wamoja,kushikana na kufanya kazi,MwanaCCM popote alipo ana jukumu la kuendelea kukijenga chama,kuwatumikia watanzania wenzetu kwa hali na mali ili mwisho wa siku ustawi wa Watanzania na taifa kwa ujumla viweze kupatikana na niwakumbushe tu kazi ya kuimarisha chama inaendelea kote nchini”,alisema. 

Katika hatua nyingine alisema jukumu la vijana wa UVCCM ni kuwalinda viongozi wa CCM na kulinda chama dhidi ya maadui nje na wa ndani ya chama /wasaliti ndani ya chama kwa sababu siyo watu wote wanaoitwa viongozi wa CCM wanania njema na CCM wengine ni vibaraka wanaotumika kuidhoofisha CCM. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack alieleza kuwa vijana wa CCM mkoani humo wapo imara na kwamba watahakikisha kuwa CCM inapata ushindi kila eneo na kwamba serikali itahakikisha kuwa Demokrasia inazingatiwa ili uchaguzi uwe huru na wa haki. 

Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele ambaye pia ni Kaimu Rais wa Bunge la Afrika (PAP),alisihi vijana kuwa na nidhamu na wavumilivu na kuwataka wanaCCM kupendana na kushirikiana huku akisisitiza kuwa CCM itashinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu. 

“Mwaka huu tutatimiza miaka 20 tangu baba wa taifa,Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere afariki dunia,nataka niwaombe Jumuiya ya Vijana tujiandae kikamilifu kufikia mwezi Oktoba,na mimi nitatoa ushirikiano wote tushangilie maisha aliyoishi Baba wa taifa,yapo mambo matatu aliyapigania ambayo ni umaskini,maradhi na ujinga hao maadui bado tunao,naomba tuendelee kupigana na maadui hawa”,alisema Masele.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: