1. Ukipiga simu mara moja au mbili halafu isipokelewe, usirudie tena kupiga mara nyingi kwani tayari unayempigia anakuwa amepata taarifa, hivyo atakupigia atakapokuwa na muda wa kufanya hivyo! Kuendelea kupiga mara nyingi si ustaarabu bali ni usumbufu.

2. Unapompigia simu mtu usiyemjua na hana namba yako ni vizuri ukaanza kujitambulisha na kueleza shida yako kabla ya kuanza kumuulizia majina yake na anakopatikana, kwani kufanya hivyo ni kukosa ustaraabu!

3. Usipende kutumia lugha zisizo rasmi katika kuwaandikia watu ujumbe mfupi wa simu. Wengine hukerwa au hawaelewi maana ya maandishi ya mtaani kama vile BC, xaxa, m2, mm nk.

4. Kabla ya kupost au kufoward taarifa yoyote kwenye magroup ya Whatsapp na facebook jifunze kusoma taarifa zilizokwisha postiwa kabla yako maana usije ukajikuta unarudia kupost taarifa iliyokwishapostiwa. Unaporudia kupost au kufoward taarifa iliyokwisha postiwa unakera na kuleta usumbufu usio wa lazima.

5. Usipende kucopy au kufoward kila taarifa bila kujiridhisha kama ni ya kweli au inatoka kwenye vyanzo vya kuaminika. Kwa mfano wengine hupost taarifa za Breaking news kumbe ni taarifa za muda mrefu au miaka mingi iliyopita.

6. Usipende kujimilikisha habari uliyocopy kwa mtu mwingine. Kila unapocopy taarifa au habari kumbuka kurejelea jina la mwandishi (Aknowlegdement) wa habari uliyocopy.

7. Usipende kujoin na kuleft magroup bila sababu za msingi. Kabla ya kujoin ni lazima ujiridhishe kama group hilo litakufaa kwa kusoma jina la group. Sio group limeandikwa "WANAWAKE TU" halafu wewe ni mwanaume na unajoin!

8. Uwapo kwenye magroup jifunze na wewe kushiriki mijadala ya masuala mbalimbali na sio kukaa kimya kama watu wasiojulikana.

9. Tumia mitandao ya kijamii kujifunza masuala mbalimbali ya kimaisha na kuelimisha wengine. Sio kila siku kazi yako ni kupost picha kuonyesha makalio, kifua, nguo ulizovaa, chakula unachokula, nyumba au ofisi za watu na magari ya watu ili tu watu wakusifie kwa coments na likes nyingi.

10. Usipende kuandika au kuacha namba yako ya simu ionekane wazi kwa kila mtu. Matapeli wengi huchukua namba kwenye mitandao na kuzitumia kwa maslahi yao.

Kama umesoma ujumbe huu mpaka mwisho basi umeelimika na bila shaka utabadilika
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: