Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakionyesha aina mifuko (vibebeo) ambayo haipaswi kutumika kuanzia leo Juni 01, 2019 baada ya kuanza kwa katazo la Serikali la uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakionyesha aina ya mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku kutumika ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala na kuachana na matumizi ya plastiki ambayo ni hatari kwa mazingira.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (kushoto) akikusanya mifuko ya plastiki iliyozuiliwa matumizi yake kutoka kwa baadhi ya akina mama wajasiriamali katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (kushoto) amesema mifuko ya plastiki ilikuwa ikisababisha uchafunzi wa mazingira hivyo wananchi wahamasike kutumia mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Mmoja wa wafanyabiashara wadogo katika eneo la "Market Street" jijini Mwanza akiendelea na uuzaji wa mifuko mbadala.
Gari la kisasa la kampuni ya usafi ya GreenWastePro linalotoa huduma ya ukusanyaji uchafu katika Mitaa mbalimbali jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wadogo waliojitokeza kupata elimu kuhusu matumizi ya mifuko mbadala kwenye zoezi la kuhamasisha katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wadogo jijini Mwanza wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu katazo la kuzalisha, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki na badala yake wajikite kwenye matumizi ya mifuko mbadala.
Wananchi na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakiwa kwenye zoezi hilo.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo pamoja na viongozi wa dini jijini Mwanza wakifuatilia wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu katazo la kuzalisha, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWestPro Kanda ya Ziwa wakiwapungia mikono wananchi baada ya kutambulishwa kwenye zoezi la kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala ambapo kampuni hiyo ni miongoni mwa wadau muhimu wa usafi na utunzaji wa mazingira.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu jijini Mwanza (kushoto), akimuonyesha Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) aina ya mifuko mbadala ambayo tayari ameanza kuiuza sokoni hapo.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu jijini Mwanza (kushoto) akieleza kuhusu upatikanaji wa mifuko mbadala na hivyo kuwatoa hofu wananchi kuhusu upatikanaji wa mifuko hiyo jijini Mwanza.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (wa pili kulia) akiteta jambo na wadau wa mazingira jijini Mwanza wakati wa zoezi la kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala na kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki.
Ujumbe muhimu unaohamasisha matumizi ya mifuko mbadaya ambayo ni rafiki kwa mazingira kutoka kampuni ya GreenWestPro inayohusika na usafi na utunzaji wa mazingira kwa sasa ikifanya shughuli zake katika mikoa ya Mwanza, Dodoma na Dar es salaam.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG.

Kampuni ya huduma ya usafi ya "GreenWastePro Ldt" imewahimiza wananchi na wafanyabiashara wote nchini kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ni adui wa mazingira na badala yake kujikita kwenye matumizi na biashara ya mifuko mbadala isiyohatarisha mazingira.

Meneja wa kampuni hiyo Kanda ya Ziwa, Salim Madafa ametoa rai hiyo leo jijini Mwanza baada ya zoezi la kuhamasisha katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki na uzinduzi rasmi wa matumizi ya mifuko mbadala. Kampuni ya GreenWestPro ni miongoni mwa wadau wa mazingira walioshiriki kwenye zoezi hilo.

"Mifuko ya plastiki imekuwa na athari kubwa katika uchafuzi wa mazingira, mitaro kujaa maji kutokana na mifuko hiyo kuziba hatua ambayo hukwamisha kazi yetu ya uzoaji taka hivyo nitumie fursa hii kuwahimiza wananchi kutumia mifuko mbadala na kuachana na mifuko ya plastiki" amesisitiza Madafa.

Baadhi ya wafanyabiashara wadogo waliokuwa wakisalimisha mifuko ya plastiki katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza, wameomba Serikali kusaidia uzalishaji wa mifuko mbadala kwa wingi na kusambazwa katika maeneo yote huku ikiuzwa kwa bei nafuu hadi shilingi hamsini (Tsh. 50) kama ilivyokuwa mifuko ya plastiki, tofauti na hivi sasa ambapo inauzwa kuanzia shilingi mia mia tatu (Tsh.300).
Tazama Video hapa chini
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: