MZIMU wa Uingereza kujitoa kwenye Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), unaendelea kuitafuna nchi hiyo ambapo leo Mei 24, 2019, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bibi. Theresa May (pichani) ametangaza kujiuzulu wadhifa huo.

Akiwa mbele ya lango la ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza 10 Downing Street leo Mei 24, 2019, Bibi May alisema, “Nimejitahidi kuwashawishi wabunge kuhakikisha suala la Brixit la (Mchakato wa Uingereza kujitoa EU), kupitia Bunge linafikia mahala pazuri lakini imeshindikana kwa hivyo sina budi kuachia madaraka ya uongozi wa chama cha Conservative ifikapo Juni 7, 2019.” Alisema Bibi May kwa majonzi makubwa.

Alisema, “Ninaondoka nikiwa Waziri Mkuu wa pili mwanamke, lakini haimaanishi nitakuwa wa mwisho, kwa heshima kubwa nimejivunia kushika nafasi ya Waziri Mkuu.” Alisema.

Hata hivyo atasalia kwenye nafasi hiyo hadi mwezi Julai atakapochaguliwa kiongozi mwingine wa chama.

Theresa May anakuwa waziri Mkuu wa pili wa nchi hiyo kujiuzulu wadhifa huo katika kipindi hiki cha msukosuko wa nchi hiyo kujiondoa katika ushirika na Jumuiya ya Ulaya, waziri Mkuu wa kwanza kukumbwa na wimbi hili alikuwa David Cameron.

Miaka miwili iliyopita David Cameron alijiuzulu baada ya wananchi wa Uingereza kupiga kura ya ndiyo ya kujiondoa kwenye Jumuiya ya Ulaya wakiushinda upande wa chama chale cha Labour kilichokuwa kinapinga Uingereza kujitoa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: