Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shinyanga Press Club. Mboneko aliwataka waandishi wa habari mkoani humo kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura ili kuchagua viongozi sahihi pamoja na kudumisha amani. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ,Shaban Alley,kulia ni Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Lutusyo Mwakyusa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwataka waandishi wa habari mkuano Shinyanga kujikita pia kuandika habari za kuchochea uwekezaji wa viwanda ili kukuza uchumi wa mkoa.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Shinyanga Shabani Alley akisoma hotuba ya Klabu hiyo siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka 2019.
Awali kabla ya kuanza kwa maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga, mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiongoza Sala ya kumuombea Mmiliki na Mwanzilishi wa Makampuni ya IPP MEDIA Dkt. Reginald Mengi ambaye amefariki dunia jana akiwa Dubai kwa matibabu.Dkt. Mengi ni miongoni mwa watu ambao wana mchango mkubwa sana kwenye Tasnia ya Habari.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Lutusyo Mwakyusa akiwahakikishia usalama wao waandishi wa habari kwenye kipindi cha uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao 2020.
Mkurugenzi msaidizi wa Radio Faraja FM Stereo Mjini Shinyanga Anikazi Kumbemba ambaye pia ni Mwandishi Mwandamizi akielezea dhumuni la maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.
Waandishi wa habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari.
Waandishi wa habari mkoani Shinyanga pamoja na wadau wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari.
Wadau wa habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.
Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga yakiendelea.
Waandishi wa habari na wadau wakiwa kwenye maadhimisho siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.
Shabani Katambi ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini akichangia mada kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mkoani Shinyanga.
Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akichangia mada kwenye maadhimisho siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuwataka waandishi mkoani Sinyanga wakijikite pia kuandika habari za kuhamasisha utalii ili Serikali iweze kupata mapato.
Diwani wa Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi (CHADEMA)akichangia mada kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mkoani Shinyanga na kuwataka waandishi wa habari mkoani humo, waandike pia habari ya kufufua kiwanda cha Nyama ambacho hakifanyi kazi katika manispaa hiyo.
Waandishi wa habari na wadau wa habari wakiendelea kusikiliza uchangiaji wa mada kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari.
Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Maguja akichangia mada kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari na kuwataka wanahabari wajikite pia kwenye maadili pale wanapokuwa wakiandika habari zao ili kuepuka kujiingiza kwenye matatizo.
Mdau wa habari Chief Abdala Sube naye akichangia mada kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari na kuvipongeza vyombo hivyo namna vinavyofanya kazi ya kutetea maslahi ya wananchi kwa kutatua kero zao.
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa 'Cheupe', akivipongeza vyombo vya habari namna vilivyosaidia kuunyosha mtaa huo ambapo ulikuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi.
Waandishi wa habari wakiwa na wadau wa habari kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari wakisikiliza uchagiaji wa mada mbalimbali.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru Chibura Makorongo akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari, na kuwataka viongozi wa Serikali waboreshe mahusiano mazuri na wana habari ili kutangaza fursa za mkoa.
Wadau wa habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.
Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments: