Wakazi wa jijini Dar es Salaam wanaotumia Mtandao wa simu wa Kampuni ya Airtel wakifanya usajili katika makao Makuu kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Usajili wa alama za vidole umeanza juzi na utaendelea hadi Decemba mwaka huu.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson MMbando akiongea na baadhi ya wateja waliojitokeza jana katika maduka ya Airtel ili kusajili laini zao kwa alama za vidole na kuwashauri kutembelea pia maduka ya Airtel huduma kwa mteja zaidi ya 20yalioko popote karibu nao pamoja na Airtel Money branch zaidi ya 600. Usajili wa alama za vidole umeanza juzi na utaendelea hadi Decemba mwaka huu.
---
*Usajili wa laini za Airtel kwa kutumia alama za vidole ni BURE kwa wote.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetangaza maduka ya Airtel maoney Branch kila kona rasmi kusajili laini za simu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole kwa mteja walioko kila mkoa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kuanza kwa zoezi hilo, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “Kama utakumbuka mwaka jana Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilizindua mfumo huu kwa majaribio. TCRA pia siku hiyo ilitoa mwongozo kwa makampuni yote ya simu kuweka utaratibu na kufanya usajili wa laini za simu mpya kwa kutumia mfumo huu mpya katika maeneo ya mikoa sita ya majaribio. Baada la zoezi hilo serikali ilitoa taarifa za kuanza usajili kwa kutumia alama za vidole kwa wateja wote. Leo hii Airtel Tanzania tunatangaza rasmi kuanza kwa zoezi hili kwenye Airtel Money Branch zaidi ya 600 pamoja na maduka ya Airtel yote bila gharama yoyote yaani BURE”
“Usajili huu wakisasa unaotumia alama za vidole ni wa uhakika zaidi na vigumu kughushi, ni muhimu sana wateja wote wapya ambao wanajiunga na Airtel kwa sasa kusaijili kwa mfumo huu’ alisema Mmbando.
Vile vile Airtel itaweka vituo maalum kwenye maeneo ya taasisi za serikali na ofisi za makampuni mbalimbali kurahizisha zoezi hili. Kadhalika, makampuni na taasisi zinaweza kuomba kutembelewa na Kitengo cha huduma kwa wateja Airtel ili kufanyiwa usajili kwenye maeneo yao ya kazi kwa kuwa sisi tunathamini muda wa wateja wetu tutajipanga na tutakwenda’ alisema Mmbando.
“Wateja wetu hasa wale wa zamani tunawasihi kuhakiki taarifa zenu za usajili kwa kupiga *106# endapo taarifa zako za usajili haziko sahihi tembelea duka letu lililopo karibu yako ili kukamilisha usajili wako kwa kutumia mfumo huu mpya wa kutumia alama za vidole” aliongeza Mmbando.
“Tunasisitiza Usajili huu ni bure na unaendelea kwenye Airtel Money Branch zote na maduka yote ya Airtel, mteja anachotakiwa kuwa nacho ili kusajili ni kitambulisho cha uraia au namba ya kitambulisho kutoka NIDA, alisema Mmbando
Tunaendelea kuongeza Maduka ya Airtel Money Branch ambayo sasa tayari yanatoa huduma kama wakala wa kawaida na pia kama wakala mkubwa ambapo hadi sasa hivi tumeshafungua matawi (Airtel Money Branch) zaidi ya 600 yanayotoa wigo mkubwa zaidi wa mawakala nchini. Ni imani yetu tutaendelea kuwafikia wateja wengi zaidi kadri muda unavyokwenda.
Toa Maoni Yako:
0 comments: