Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wazazi pamoja na Wadau waliofika katika Maadhimisho ya siku ya Usonji
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Zawadi kutoka kwa Azim Dewji mara baada ya kushiriki Matembezi ya siku ya Usonji
Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete akikabidhi Zawadi ya Picha kwa Mmoja ya Wazazi wa shule hiyo ambao walinunua kama ishara ya kuchangia Watoto wenye Usonji.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akiongoza Matembezi ya kuchangia Watoto wenye Usonji wanaosoma katika Shule ya Al Muntazar.
Rais Mstafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza Matembezi ya Wazazi na Wanafunzi wa Shule ya Al Muntazar.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wazazi na walezi kutowaficha ndani watoto wenye Usonji kwa kuwa wanauwezo wa kufundishika.
Akizungumza baada ya matembezi hayo Dkt. Kikwete amesema ugonjwa wa usonji umeenea duniani kote kwa wananchi matajiri na masikini, lakini pia unaitaji uvumilivu kwa wazazi na walezi kwa kuwa ugonjwa huo unaitaji uangalizi wa hali ya juu wakati wote.
"Watoto hao wanategemea sana mapenzi ya wazazi na walezi na jamii kwa ujumla, pia wanategemea kulindwa kwasababu wasipolindwa na kuangaliwa wanaweza hata kujiumiza wenyewe"amesema
Aidha ameipongeza Bodi ya shule ya Al Muntazir ambayo imeanzisha shule maalumu ya watoto wenye mahitaji maalumu ikiwemo Usonji ambao wamekuwa wakiwapatia mafunzo mbalimbali ya vitendo pamoja na Elimu.
Dkt. Kikwete ametoa wito kwa wizara husika ikiwemo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto na makundi mbalimbali kwenye jamii kutambua tatizo hilo na kuchukua hatua ya kutoa elimu kwa jamii,katika kuelimisha malenzi kwa watoto hao na nini kifanyike ili kuweza kuwasaidia watoto wenye maradhi ya Usonji.
Aidha amesema jitihada hizo ziongezwe mara dufu kwa kuwekeza elimu kwa jamii ili waweze kutambua ugonjwa wa Usonji,pia ameiomba jamii kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na shule ya Amsen ili mradi huo uweze kufanikiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shule za Al Muntazir Imtiaz Halji amesema njia bora ya kuwaonesha watoto wenye mahitaji maalumu ni kuwalinda na kuwapenda na kuacha tabiya ya kuwatenga ili wasishirikiane na wenzao.
“Wakati sasa umefika tuunganishe nia zetu kuelekea lengo moja,kufanya kila kitu kilicho ndani ya uwezo wetu kuunga mkono katika kuelimisha jamii ” amesema
Toa Maoni Yako:
0 comments: