Na Mwandishi Wetu.

MABONDIA Hussein Pendeza na Juma Ramadhani 'Choki' wametamba kila mmoja kwa wakati wake juu ya mpambano wao utakaofanyika April 21 siku ya sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu Magomeni Mapipa, Dar es Salaam.

Akizungumza kuhusu mpambano wake Juma Ramadhani 'Choki' amesema kuwa kwa sasa yani yupo fit mpaka yeye mwenyewe anajiogopa kutokana na mazoezi anayofanya kwani nimefanya mazoezi ya kutosha na nipo tayali kwa mpambano na yoyote yule sio huyu peke yake bondia yoyote yule alie katika uzito wangu nita akikisha nampiga kipigo cha mbwa mwizi kwa hivyo kaeni chonjo vinginevyo nitawalalawa laluwa na sijaona katika uzito wangu wa kg 58 wa kunisumbua kwani ninajiamini na nina amini mazoezi ninayo yafanya.

Choki amewaomba mashabiki wake wa Manzese, Mabibo pamoja na Mbagala kuu na Mtoni Kijichi wajitokeze kwa wingi kuja kumpa sapoti siku hiyo na wangalie nini anafanya katika mchezo huu wa masumbwi nchini.

Nae Pendeza amesema kuwa atahakikisha anampiga kama beg kwa Juma ni mtoto mdogo sana katika masumbwi hivyo atajuta kuzaliwa kwa kipigo nitakacho mpatia siku hiyo. 

Pendeza ameongeza kwa kuwaomba mashabiki wake wote na wapenzi wa ngumi kujitokeza siku hiyo kuangalia jinsi anavyo msambalatisha kijana huyo.

Mpambano huo ulioandaliwa na Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa pambano hilo litafanyika siku ya sikukuu ya Pasaka likiwa limepewa nguvu na 
Bondia Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini Australia bondia huyo ndiye aliyesababisha mabondia hao wazipige siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndiyo maana akaongeza nguvu ili mpambano huo ufanyike.

Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika siku hiyo ambapo bondia Idd Mkwera ataonyeshana umwamba na Rojas Masamu na Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede wakati Ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atakabiliana na Rashidi Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Shabani Mbogo Hussein Shemdoe na Shehe Azizi na Ahmadi Kombo atakumbana na Sandali Nyambala.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: