Mkurugenzi wa mikopo kwa wateja wakubwa Goodluck Nkim akiwaelezea wanahisa faida za kununua hisa katika benki ya CRDB na namna ambavyo wametoa nafasi kwa wanahisa kuelewa Zaidi uwekezaji wa viwanda na kuwaeleza kitu gani wanaweza kufanya ili kufaidika na myororo wa uchumi.
Wanahisa wakijisomea kilichoandikwa kwenye makablasha waliopewa mara baada ya kujisajili kushiriki mafunzo ya wanahisa na Benki ya CRDB mkoa wa Morogoro .
Wafanyakazi wa benki ya CRDB mkoa wa Morogoro wakifatilia kwa makini mada zinazotolewa na wawezeshaji katika mafunzo ya wanahisa mkoani Morogoro.
Meneje wa bank ya CRDB tawi la Mzumbe mkoani Morogoro Jane Maganga akiteta jambo na Meneja wa mikopo CRDB Denis Kayanda nje ya mkutano .
Wanahisa wa benki ya CRDB mkoa wa Morogoro wakisajiliwa na wafanyakazi wa bank hiyo ili kupokea makablasha ya mkutano kabla ya kuanza mafunzo yaliyolenga kuwa elimisha namna ya kuchangamukia fursa mbali mbali zinazo wezakujitokeza kwenye uwekezaji wa viwanda.
Mkurugenzi wa benki ya CRDB mkoa wa Morogoro Lusing Sitta akiteta jambo na Meneja wa CRDB tawi la Mandela mkoa wa Morogoro Stephen Mapunda wakati wa mkutano baina ya benki na wanahisa wa benki hiyo.
Wafanayakazi wa CRDB wakiwasikiliza kwa makini wanahisa waliohitaji kujisajili na kupewa kablasha zao zinazoonesha vipengele vya mafunzo ya wanahisa na vyeti vya kuthibibisha kuwa ni wanahisa.
---
Benki ya CRDB mkoa wa Morogoro imeamua kushirikiana na serikali katika kuhamasisha wananchi kuchangamkia fursa mbali mbali kujitokeza kwenye uwekezaji wa viwanda ili kuendana na matakwa ya sera ya nchi katika mpango uliopo wa miaka mitano . 

Akizungumza mara baada ya semina ya wanahisa wa bank ya CRDB mkoa wa Morogoro iliyolenga kuwa elimisha wanahisa na wananchi wengine fursa mbalimbali za kiuchumi na mambo yanayohusu Benki hiyo .

Mkurugenzi wa wateja wakubwa Bank ya CRDB Goodluck Nkim amesema wametoa nafasi kwa wanahisa kuelewa Zaidi uwekezaji wa viwanda na kuwaeleza kitu gani wanaweza kufanya ili kufaidika na myororo wa uchumi hii ikiwa ni njia Mojawapo ya CRDB kuonesha mchango wake katika ujenzi wa viwanda huku Mkurugenzi wa benki ya CRDB mkoa wa Morogoro Lusingi Sitta amewataka wananchi kujisajili katika ununuzi wa hisa kwenye bank hiyo kwani umilikiwa hisa unafaida mbali mbali ikiwemo kukuza kipato cha mtu binafsi na makampuni. 

Aidha washiriki wamepongeza utoaji wa mafunzo hayo yaliyoweza kuongeza uwelewa wa wanahisa na kuiomba bank iweze kujitanua Zaidi katika kukopesha wanahisa walioko katika vyama mbalimbali vya wakulima ,kuelimisha Zaidi maana ya viwanda na kutengeneza jambo endelevu kwa ajili ya wastafu ambao sasa hivi ni wanahisa wa bank ya CRDB baadala ya kufikilia kuwakopesha. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: