Kampuni maarufu ya kimataifa yenye asili ya Asia ya mauzo ya moja kwa moja, QNET inaendesha kongamano la siku tano la kimataifa ambalo linaleta pamoja takribani wajasiriamali 13,000 kutoka maeneo mbalimbali duniani katika kisiwa cha Penang

Kongamano lenye hamasa litashuhudiwa na wasambazaji wa QNET kutoka katika zaidi ya nchi 30 watakao kutana pamoja katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa na maonyesho wa Subterranean Penang International Conference & Exhibition Centre (SPICE) katika mji wa Bayan Baru, Penang, Malaysia

Shughuli za ufunguzi wa sherehe zilifanywa na Yang Berhormat Profesa Dr. P. Ramasamy, Naibu Waziri Kiongozi II wa Penang, Mwenyekiti Mtendaji wa QI Group, Dato Sri Vijay Eswaran na Kaimu Naibu Mwenyekiti Joseph Bismark. Vile vile walikuwepo Mh. Cissé Ibrahim Sory, Meneja Mkuu wa Guinea Microfinance Agency ANAMIF, na washirika wengine wa biashara za kimataifa wa QNET kutoka Afrika, na sehemu mbalimbali duniani. 

Kongamano hili ambalo linajulikana kama V-Malaysia 2019 limefanyika Penang kwa miaka sita mfululizo. Wateja na wasambazaji kutoka katika masoko makubwa ya kikanda ya QNET katika Mashariki ya Kati, Katikati ya Asia, Afrika, Bara Hindi, Indonesia na Malaysia wanahudhuria kongamano la mwaka huu. Kongamano la siku tano litajumuisha mfululizo wa programu za mafunzo, hotuba za uhamasishaji, kutambulisha bidhaa mpya za mtindo wa maisha wa QNET na burudani. Kivutio kikubwa mwaka huu ni QNET Carnival ambayo itaonyesha zaidi ya nembo au lebo 50 za bidhaa za QNET katika moja ya maonyesho makubwa kuwahi kufanywa na kampuni hiyo. 

Katika hotuba yake, Naibu Waziri Kiongozi II wa Penang Profesa Dr. P. Ramasamy alitoa shukurani zake kwa QNET kwa kuja Penang kwa miaka sita mfululizo na kufanya kongamano kubwa la siku tano. 

"Ningependa kusisitiza kwamba Penang inajulikana vyema kwa ari yake ya ujasiriamali na kwa kutengeneza wajasiriamali kwa miaka mingi nchini. Ninahakika kwamba QNET itasaidia kuhamasisha wajasiriamali wa leo kuwa chombo cha mabadiliko ya kesho," alisema Dr. P. Ramasamy na kufuatia na shangwe za nguvu na makofi kutoka kwa wasambazaji wa QNET kutoka sehemu mbalimbaloi duniani. 

Mkurugenzi Mkuu wa QNET Bwana, Malou Caluza alisema: "Matukio kama haya ya Kongamano - V (V-Convention) linatupa fursa ya kuwahudumia wasambazaji wetu na kuwaruhusu kuwa na sisi kwa karibu. Tumewaleta takribani wafanyakazi 250 kutoka katika maeneo mbalimbali duniani kutusaidia katika kongamano hili na kuwapa washiriki wa kongamano hili uzoefu wa hali ya juu. Vile vile ni jukwaa bora la kusherehekea ari ya ujasiriamali ambayo kampuni ya mauzo ya moja kwa moja kama QNET inachochea kwa mamilioni ya watu duniani kote, kuwasaidia kuboresha maisha yao na kuchangia katika jamii." 

Akiongeza katika hilo, Meneja Mkuu wa QNET wa eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara bwana M. Biram Fall alisema: "V - Malaysia inafuatilia kongamano lenye mafanikio 2019 la msimu wa QNET Expo lililokuwa linajulikana kama Absolute Living, sambamba na misingi ya kampuni ya mauzo ya moja kwa moja na falsafa ya RYTHM - Raise Yourself to Help Mankind – inayofanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani kote ikiwa na lengo la kuonyesha bidhaa na huduma zake zilizoko sokoni ambalo lilianza mwaka 2019 jijini Dar es salaam, Tanzania mwezi uliopita, kisha kuhamia jijini Kumasi, Ghana na baadae katika nchi nyingine za Afrika. 

QNET, Kampuni tanzu inayoongoza ya kundi la makampuni la QI (QI Group of Companies), inauza reja reja bidhaa mbalimbali za Afya na ustawi, huduma binafsi na urembo, sikukuu, utunzaji wa nyumba na kozi kwa njia ya mtandao miongoni mwa nyingi zingine ambazo zinaboresha maisha ya kila siku ya wateja wake duniani kote. QNET iliwekwa katika moja kati ya makampuni 100 makubwa na imara ya MLM (Solid Top MLM Companies) kwa mwaka 2018 na Portal ya habari za mauzo ya moja kwa moja ya Business for Home.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: