Na Mwandishi Wetu
Shirika la Legal Services Facility (LSF) jane limetangaza rasmi uteuzi wa Bi Lulu Ng’wanakilala kama Ofisa Mkurugenzi Mkuu mpya. Katika kutekeleza kazi hii, anachukua nafasi ya Bw Kees Groenendijk, ambaye ameongoza asasi hii tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011.
Bi Ng’wanakilala, ambaye ana Shahada ya Pili katika Sheria ya Kimataifa na Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Livraserpool nchini Uingereza na Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, amedhamiria kufanya mabadiliko ya kitaasisi lengo kuu likiwa ni kuifanya LSF kupanua wigo utoaji wa msaada wa kisheria kwa mamilioni ya wanaume na wanawake maskini Tanzania wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.
Anachukua uongozi wa asasi isiyo ya kiserikali ambayo imewezesha uwepo wa wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar, wanaotao msaada wa kisheria kwa watanzania wenye matatizo ya kisheria na kuwawezesha kupata haki zao.
Akitoa mtazamo wake, Afisa Mkurugenzi anayemaliza muda wake, Bw. Mkurugenzi Bw Groenendijk, anasema: “Tangu mwanzoni kwa msaada wa washirika wa maendeleo DANIDA naDfID, LSF imefanya kazi kubwa ya kuweka mazingira yaliyowezesha upatikananji wa huduma za kisheria kwa watu maskini hasa wanawake, kuwa rahisi na wakuaminika.”
Kwa kupitia mtandao mkubwa wa takriban wasaidizi wa kisheriahai 3,000 nchi nzima, “tumeweza kuleta mabadiliko chanya kwa maisha ya watu maskini, mpaka kwa wale waishio wa pembezoni. Kwa umuhimu unaofanana ni ukweli kwamba LSF inafanya kazi na asasi zingine za kiraia na serikali kuwezesha mabadiliko ya sera na sheria kwa lengo la kuhakikisha haki inabakikuwa sifa muhimu ya maisha ya kila siku ya mamilioni ya Watanzania. Ofisa Mkurungenzi Mkuu mpya atakuta misingi bora yenye lengo la kutekeleza maono yake, na hatimae kukuboresha misingi na maono hayo zaidi na zaidi.”
“Ng’wanakilala analeta nguvu na kasi mpya ya uongozi wenye mawazo mapya, uzoefu na maarifa mapana aliyonayo katika taaluma na nyadhifa mbalimbali alizoshika ambazo ni muhimu katika kuipeleka LSF mbele na kuwawezesha maelfu ya wananchi kuendelea kupata na kutambua hakizao,” anaongezaBw Groenendijk.
Akimkaribisha Ofisa MkurugenziMkuumpya, Mwenyekiti wa Bodiya LSF, Dk Benson Bana anasema: “Huduma za kutoa msaada wa kisheria ni kiini kinachoelezea kazi ya LSF. Kwa miaka hii michache asasi hii imebadilisha maisha ya watu wengi wa kawaida kwa kutilia mkazo kuwainua wanawake ambao kwa mfumo dume uliopo wamekuwa hawafaidiki sana. LSF, kwa ushirikiano kutoka serikalini, inaendelea kuwezesha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kila siku bila malipo yoyote. Ofisa Mkurugenzi Mkuu anayekuja ataunganisha vizuri watu hawa na kwa kutumia utajiri wa uzoefu wake ataweza kuiwezesha LSF kukuza fursa kwa watu wengi zaidi kunufaika na kujitoa kwetu kwa upatikanaji wa haki.”
Kabla ya uteuzi wake LSF, Ms Ng’wanakilala alishika nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Mtandao wa UtepeMweupe kwa Uzazi Salama Tanzania (WRATZ), mjumbe wa KamatiyaUtendajiyaMradiUnaoongoza wa Uamzi Salama (LSC), Mkurugenzi wa BodiyaWanawake wa Mafanikio Tanzania (TWA) namwanzilishinamjumbe wa BodiyaKituo cha MawasilianonaMaendeleo Tanzania (TCDC).
Amefanya kazi kubwa katika mabadilikoya sera na kwenye vikundi vya kitaalamu vinavyoratibu, wezesha na ameshiriki katika hatua mbalimbali za utekelezaji, ikiwani pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupungu za Umaskini Tanzania (Mkukuta). Bi Ng’wanakilalanimwanachama pia wa Chama cha WanasheriaTanganzania Bara (TLS).
Uteuzi wa Bi Ng’wanakilalaunaanzarasmi Mei 1, 2019.
Toa Maoni Yako:
0 comments: