Meneja wa huduma kwa wateja wa DAWASA Doreen Kiwango akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya wiki ya Maji Duniani ambapo DAWASA wameweka dawati kwa ajili ya kusikiliza kero na maoni ya wateja wao.
Mkurugenzi wa Manunuzi DAWASA, Hellen  Lugongo akizungumza na wanahabari jijini Dar es  Salaam wakati akielezea mamlaka hiyo imejipanga kutekeleza miradi mbalimbali ili kuweza kuwapatia wananchi majisafi na salama.
Watoa Huduma wakiendelea kutoa elimu na kutatua kero za wananchi waliofika katika Wiki ya Maji Duniani inayoadhimishwa na DAWASA kwa kusikiliza kero za wananchi katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam iliyoanza Machi 16-22, 2019.
Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Neli Msuya akitoa elimu na kutatua kero ya mwananchi aliyefika katika Wiki ya Maji Duniani inayoadhimishwa na DAWASA kwa kusikiliza kero za wananchi katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam iliyoanza Machi 16-22, 2019.
Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Neli Msuya akizungumza na Mkurugenzi wa Manunuzi DAWASA, Hellen  Lugongo mara alipotembelea katika Wiki ya Maji Duniani inayoadhimishwa na DAWASA kwa kusikiliza kero za wananchi katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam iliyoanza Machi 16-22, 2019.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa DAWASA, Evelasting Lyaro akitoa elimu na kutatua kero ya mwananchi aliyefika katika Wiki ya Maji Duniani inayoadhimishwa na DAWASA kwa kusikiliza kero za wananchi katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam iliyoanza Machi 16-22, 2019.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam  (DAWASA) imejipaga kuwahudumia wananchi wa jiji la Dar es Salaam na Pwani kwa kuendelea kuwapa huduma ya MajiSafi na Salama.

 Imetoa angalizo kwa wateja wake kuepuka kulipa malipo yoyote  kwa Mamlaka hiyo kwa njia fedha taslimu na simu za watu binafsi bali watumie utaratibu  wa malipo walioelekezwa.

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya maji, Meneja wa huduma kwa wateja Doreen Kiwango amesema fedha za malipo za DAWASA zinapitia katika  mfumo wa malipo wa serikalic (GePG).

"Niwaombe wateja wetu wote ukikutana na mfanyakazi anayetaka malipo kwa njia ya fedha taslimu ama simu yake ya mkononi toeni taarifa DAWASA ili achukuliwe hatua za kisheria," amesema Kiwango.

Amengeza kuwa hata kama mteja wa DAWASA ulikatiwa huduma unatakiwa kulipa kupitia mfumo wa malipo ya Serikali.

"DAWASA hatupokei fedha taslimu hivyo watumie namba (control number) walizopewa katika malipo ama mtandao sahihi walioelekezwa," amesema Kiwango.

Amesema kwa sasa wakazi wa Pugu na Gongolamboto watarajie kupata huduma ya uhakika ya Majisafi kwa kuwa DAWASA inajenga tenki litakalohudumia maeneo hayo.

"Tumejipanga kuhakikisha wakazi wote wa pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam na Pwani wanapata huduma ikiwa ni pamoja na Saranga, Kisukuru, Salasala na maeneo mengine," amesema Kiwango.

Ameongeza kuwa kwa sasa DAWASA kwasasa inatoa huduma ya maunganisho ya maji kwa mkopo hivyo wananchi ambao hawana huduma hiyo wafike katika ofisi za mikoa.

Naye Mkurugenzi wa Manunuzi DAWASA, Hellen  Lugongo amesema mamlaka hiyo imejipanga kutekeleza miradi mbalimbali kwa kasi waliojiwekea.

"Idara ya Manunuzi inatumia sheria ya Manunuzi ya mwaka 2016 kutekeleza miradi hiyo kwa kasi kulingana na mahitaji ya mipango tuliyojiwekea ," alisema Hellen.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: