*Wananchi waelimisha zaidi faida za matumizi ya huduma ya EzyPesa
Wafanyakazi wa Zantel wameshiriki katika zoezi la usafi katika masoko ya kuuza mazao ya Ilala jijini Dar es Salaam na Saateni Zanzibar na kutoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa masoko hayo ikiwa ni moja ya mkakati wa kampuni hiyo kuwajibika na kujitoa kwa jamii.
Kupitia zoezi hili Zantel ina lengo la kuhamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kusafisha maeneo wanayofanyia biashara, kuhifadhi mazingira pamoja na kuelimisha jamii kuhusu madhara ya uchafu na takataka kiujumla.
Mbali na kufanya usafi wafanyabiashara wa katika masoko hayo na wananchi wanaoishi jirani na maeneo hayo walipata fursa ya kuzifahamu huduma zinazotolewa na Zantel ikiwemo huduma ya fedha kupitia mtandao wake ya EzyPesa ambayo inarahisisha maisha kutuma na kupokea fedha sambamba na kufanya mihamala ya malipo ya huduma mbalimbali.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Zantel wakifanya usafi katika soko la Ilala jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi kwa uongozi wa soko hilo.
Meneja Mauzo wa Zantel Kanda ya Zanzibar, William Damas Chama akikabidhi vitendea kazi ya safi kwa mfanyakazi wa Manispa ya Zanzibar, Jina Mohamed Vuai (kulia) aliyepokea kwaniaba ya Mkuu wa soko la Saateni.
Wafanyakazi wa Zantel wakiwa katika kazi ya usafi kwenye soko la Saateni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Mkuu wa Mauzo wa Zantel Tanzania kanda ya Dar na Pwani, Emmanuel Joshua (Kulia) akimkabidhi Meneja wa Soko la Ilala jijini Dar es Salaam, Selemani Mfinanga vifaa vya fanyia usafi wakati wafanyakazi wa Zantel Tanzania walipokwenda kufanya usafi katika maeneo ya soko hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: