Mshindi wa mbio za KM 21, Emmanuel Giniki (wa mbele) akichuana na Mkenya Bernard Musau katika mbio za Kilimanjaro zilizofanyika Kilimanjaro, Moshi. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.


Mpambano mkali.
Habari na Vero Ignatus, Kilimanjaro.

Mashindano ya 17 tangia kuanza mbio za kilimarathoni yamefanyika mkoani kilimanjaro katika uwanja wa ushirika na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya elfu kumi

Mashindano hayo yameshirikisha mataifa zaidi ya 50 kutoka ndani na nje ya Taifa la Tanzania ambapo walianza na mbio za kilometa arobaini na mbili, ishirini na moja na kilometa tano

Katika mbio za kilometa 42 upande wa wanaume mshiriki mwenye namba (1) 606 Cosmas Muteti 2:18:27, 321 David Kipkorir Rutoh 2:18:48, 476,Robert Okunde (Uganda) 2:18:48 , ambapo Tanzania imeshika namba 8 kutoka Stephano Huche mwenye namba 580 ya ushiriki ametumia 02:22:54

Kwa upande wa wanawake mshiriki mwenye namba (1) 518 Lydia Nasimiyu Wafula 2:52:17,(2)240 Monica Cheruto 2:58:00 (3) Teclah Chebet 3:8:57 wote hawa kutoka nchini Kenya ,kwa upande wa Tanzania mshiriki mwenye namba 310, Baanuelia Katesigwe amekuwa 8 anetumia 3:23:26

Mbio za kilometa 21 Mtanzania Emmanuel Giniki ameibuka kidedea kwa kutumia 01:03:34, wapili Bernard Musau (Kenya) 1:03:42, Joseph Njenga Njihia 1:5:13 (Kenya).

Kwa upande wa wanawake ameongoza mshiri mwenye namba 4564(kenya)1:11:45,kutoka Tanzania mshiriki namba 2103 Failuna Abdi Matanga 1:14:1,Ester Chesang Kakuri 1829 anetumia 1:14:42(
kenya)

Waziri wa habari, Utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Chama cha mchezo cha riadha nchini hakina mpangiliao mzuri wa michezo na amesema ataitisha kikao kwaajili hiyo na kuhakikisha kuwa ratiba inazingatiwa ili kuwe na ufanisi mzuri.

'' Leo hii kuna mbio nyingine kama majeshi zinaendelea jijini Dar es salaam, hivyo imewanyima haki wanariadha wengi kushiriki tutakaa tuwe na mipango ya pamoja''Alisema Mwakyembe

Amesema amepoka changamoto kubwa ambayo ni barabara kuwa nyembamba hivyo wanariadha kushindwa kuwa na upana katika kujituma wakiwa katika mbio hizo

Aidha Waziri wa habari utamaduni, sanaa na michezo Dkt Harryson Mwakyembe amewapongeza wale wote waliofanya vizuri katika marathon na nusu marathoni

Antoni Mtaka Rais wa Riadha nchini amesema kuwa Shirikisho la Riadha la Afrika wamewapa jukumu la kuandaa mbiyo za nyika Afrika ambazo zitafanyika mkoani Kilimanjaro na wanategemea kuwa na washiriki kutoka nchi zaidi ya 54 duniani

'' Hivyo wana Kilimanjaro jiandaeni na ugeni huo na pia mjiandae kufanya biashara zaidi kuliko hivi leo. Alisema Mtaka"alisema Mtaka

Akizungumza mshiriki wa mbio km 21 Hans Leonard amesema kuwa changamoto kubwa waliyokumbana nayo ni barabara kuwa nyembamba hivyo wanariadha wengi kushindwa kukimbia kwa wakati mmoja

Kwa mujibu wa Meneja maendeleo ya biashara kutoka kampuni ya AAR Healthcare Dosca Masama amesema Changamoto iliyoonekana katika mashindano hayo ni washiriki wengi kutokuwa na mazoezi ya kutosha hivyo kusababisha kukaza kwa misuli wakati wakikimbia na wengine kuishiwa pumzi

''Ni mara yetu ya pili kufadhili mbiyo washiriki wengi wamepata muamko ila tumekutana na changamoto ya washiriki kurudi wakiwa wamechoka sana, misuli imekaza,wengine wamezimia barabarani wakiwa wanatembea''Alisema

Amesema wamepokea zaidi ya washiriki 500 ambao wamewapatia huduma na wale ambao wapo nje ya uwezo wao wamewapeleka hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi

Naye mshindi wa mbio za nusu marathoni Kilometa 21 Immanuel Giniki amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kumsaidia kushinda mbio hizo kwani ushindi siyo wa kwake pekee ni wa Taifa lake kwa ujumla.

Immanuel Giniki ni mara yake ya tatu kushiriki katika mashindano hayo ambapo mwaka 2015 alishika nafasi ya pili 2016 akawa wa kwanza na 2019 ameshika tena nafasi ya 1
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: