Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipongeza Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya I CAN ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee kwenye hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akipokea hundi ya sh.milioni mbili kutoka kwa mwakilishi wa Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akizungumza na Michuzi Blog wakati hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka.MMG)
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na watu wenye ulemavu mara baada ya ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akiwa katika picha ya pamoja na Familia yake katika ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka- MMG).

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 

Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh amesema kuwa jamii iache kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu kwani watu wenye ulemavu wanaweza kufanya vitu vikubwa na kusaidia nchi katika maendeleo mbalimbali.

Nuru aliyasema hayo wakati wa hafla ya Tuzo ya I Can ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Nuru amesema Tuzo mbili alizozipata zimetokana na kuwa na mchango katika jamii licha ya kuwa na ulemavu wa kuona lakini ameweza kutumia kipaji chake na kuiletea maendeleo nchi pamoja na wananchi.

Amesema kuwa yeye angefungiwa ndani asingeweza kupata elimu na kufanya maisha yake ya ulemavu kufunga kipaji pamoja na ndoto zake ambapo leo anaongoza watu wa makundi mbalimbali na wanamuamini katika uongozi.

‘’Namshukuru Rais Dkt. John Pombe Mgufuli kwa kuteua viongozi mbalimbali wenye ulemavu katika serikali yake ni kutokana na kutambua mchango wa wenye ulemavu kushiriki katika ngazi za maamuzi na sasa kufanya walemavu kijiamini kwa kupita kifua mbele”.amesema Nuru.

Nuru amesema watu wenye ulemavu wana kipaji kikubwa huvyo jamii iache kuwafungia ndani kwa kuona hawawezi kufanya chochote katika jamii yao wanayoishi.

Aidha amesema kuwa watu wenye uleamvu kwa vijana wanaosoma wasife moyo kwa ulemavu wao wasome kwa bidii kwani elimu ndio mkombozi kwa mtu mwenye ulemavu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: