WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kutembelea wilaya ya Kilindi wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo.
Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua akimueleza changamoto ya maji ya wilaya hiyo Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa wakati alipofanya ziara wilayani humo 
MKUU wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa.
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akitoka eneo la mradi mara baada ya kulikagua wakati wa ziara yake wilayani Kilindi kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo.
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa amempa muda wa siku nne Mkandarasi wa Kampuni ya Sajo Octavious Nduke kuhakikisha mradi wa maji wa Bokwa uliopo eneo la Mabobwe wilayani Kilindi unakamilika na wananchi waweze kunufaika na huduma ya maji ndani ya wakati huo.

Mradi huo ambao umegharimu zaidi ya sh.milioni 300 ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2017 na ulitakiwa kukamilika mwaka jana ili kuweza kutoa maji na kuondoslkha kero kwa wananchi hao hata hivyo baadae maji hayakuweza kulikotokana na changamoto mbalimbali.

Alisema hayo mara baada ya kuutembelea na kuzungumza na wananchi ambapo alisema iwapo mkandarasi huyo atashindwa kufanya kazi hiyo kwa kipindi hicho ambacho amemwaagiza yeye anajua wapi atakwenda kuchukua fedha ili waweze kuwanunuliwa mota ambayo itafungwa ili wananchi waweze kupata huduma ya maji ili kuondokana na kero zilizopo

“Lakini pia nikuambie kama hautanunua mota hii wala usisubutu kuomba kazi nyengine kwa sababu utakuwa umetutapeli ….hauwezi kuendelea kula fedha wakati wananchi wanaendelea kuteseka hii haikubaliki akifanya ujuaji mimi najua mahali pa kwenda kuchukua fedha tuna fedha yake tumeizuia akifanya kupindisha tunachukua hela tunanunua mota muweza kupata maji “Alisema Waziri Mbarawa.

“Nendeni mpaka Ijumaa mhakikishe mmekwisha kununua mota na kuifunga hapa wananchi waweze kupata huduma ya maji kutokana na kwamba mradi huu ulikuwa kwenye muda wa matazamia hivyo ikitokea chochote kimeharibika kwenye miundombinu hii ndani ya mwaka mzima atalazimika kutengeneza kwa fedha zake za mfukoni na ndio maana ya muda wa matazamia”Alisema

Awali akitoa taarifa za mradi huo wakati wa ziara hiyo, Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya Sajo, Octavious Nduke alisema mradi huo tayari ulishakamilika kwa asilimia mia moja na wananchi wakaanza kupata maji lakini baadae ikajitokeza changamoto ya kuungua kwa vifaa.

“Mh Waziri katika mradi huu maji yalikuwa yanatokana na wananchi kuweza kuyapata lakini kuna changamoto ya kuungua baadhi ya vifaa na hivyo kupelekea kukwama kuendelea kutoa maji lakini tutalifanyia kazi “Alisema

Akijibu changamoto hiyo Waziri Profesa Mbarawa alisema suala la kununua vifaa vilivyoungua ni jukumu la mkandarasi hivyo kumtaka afanye hivyo mara moja ili kuwaondolea wananchi adha wanazokumbana nazo.

Naye kwa upande wake Diwani wa kata ya Bokwa Idirisa Mgaza alimueleza Waziri huyo kwamba mradi huo umewapa shida kama viongozi huku wananchi wao wakiendelea wanataabika juu ya suala la upatikanaji wa maji.

“Mh Waziri tunaomba tatizo hili uone namna ya kulipatia ufumbuzi kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa eneo hilo wanaonekana na changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji “Alisema.

Katika hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Kilindi Omari Kigua amemuomba waziri Mbarawa kuwapelekea fedha kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji ambao utakuwa mkombozi wa changamoto ya maji kwenye wilaya hiyo ambapo waziri ameahidi kulifanyia kazi.

Alimueleza waziri huyo kwamba suluhu ya ufumbuzi wa changamoto ya maji wilayani humo ni mradi mkubwa wa maji kutoka Mto mkubwa Pangani au Ruvu Korogwe yafika hadi makao makao makuu ya wilaya yatasaodoa kuondokana na adha wanayoipata kwa sasa.

“Lakini maji hayo yatakapofika makao makuu ya wilaya yanaweza kufika kwen ye vijiji mbalimbali kwa urahisi na hivyo wananchi kuweza ,kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa maisha ya kila siku “Alisema
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: