Naibu Waziri – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Dkt. Mary Mwanjelwa akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa Meneja mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Glory Mziray aliyefariki dunia juzi mchana Jumanne Februari 19, 2019 ibada ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika kwenye kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam leo.

Mwili wa Marehemu Grory Mziray umesafirishwa kwenda nyumbani kwao Mikese mkoani Morogoro ambako utazikwa kesho inatoa pole kwa familia ndugu na jamaa na marafiki kufuatia msiba huo, Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu Grory Mziray -AMEN.
Mume wa Marehemu Grory Mziray akiwa na watoto wake wakilia kwa uchungu kufuatia kifo cha ghafla cha mke wake kilichotokea jumanne wiki hii akiwa kazini kwake.
Mume wa Marehemu Grory Mziray akiwa na watoto wake wakiaga mwili wa marehemu mama yao kufuatia kifo cha ghafla cha mke wake kilichotokea jumanne wiki hii.
Afisa habari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Bw. Prosper Minja akiaga mwili wa marehemu Grory Mziray.
Bw. Yohana Mtweve akiongozana na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Grory Mziray.
Wanahabari kutoka Ayo Tv Mika Ndaba na Dalla ni miongozi mwa waombolezaji waliofika kuaga mwili wa marehemu Grory Mziray.
Afisa habari kutoka Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Twaha John akishiriki kuaga mwili wa marehemu.
Tulizo Kilaga mmoja wa watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) akiaga mwili wa marehemu.
Watoto wa marehemu Grory Mziray na ndugu jamaa na familia wakiongoza wakati mwili wa marehemu ukitolewa kanisani tayari kwa safari ya kuelekea Mikese mkoani Morogoro ambako marehemu atapumzishwa
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Grory Mziray ukitolewa kanisani tayari kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea mkoani Morogoro kwa mazishi.
Waombolezaji wakibeba mwili wa marehemu Grory Mziray ili kupakia kwenye gari.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: