Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad



Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) ameipongeza serikali ya awamu tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kuzipatia fedha shule zenye msongamano mkubwa wa wanafunzi katika halmashauri ya Shinyanga. 

Azza ametoa pongezi hizo jana Februari 21,2019 kwenye Mkutano wa hadhara wa wananchi wa kata ya Tinde iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga uliohudhuriwa pia na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko. 

Alizitaja shule zilizopokea pesa kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa madarasa,vyoo na nyumba za walimu kuwa ni Shule ya Msingi Masunula (Milioni 146.6),Mwasingu (milioni 46.6),Tinde A (milioni 46.6) na Tinde B (milioni 46.6). 

Mbunge huyo aliishukuru serikali kwa kazi nzuri iliyofanya tena kwa muda mfupi kusikia kilio cha wananchi wa Shinyanga huku akibainisha kuwa aliombea shule nyingi za mkoani Shinyanga zilizopata sasa ni hizo shule nne. 

“Mheshimiwa DC upo hapa kwa niaba ya Mheshimiwa Rais,nitumie fursa hii kuishukuru sana serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli,serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi,serikali sikivu,nimesema wamenisikiliza kwa muda mfupi,nifikishie salamu hizi”. 

“Tunashukuru sana kwa kutusikiliza Wana Tinde,Jukumu langu kama Kiongozi ni kubeba kero zenu na kuhakikisha nawasemea na kuzitatua ninaamini lile goti mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nikazisemea shule zenye msongamano mkubwa wa wanafunzi,Mwezi Julai 2018 alipopita Tinde lilikuwa linatoka ndani ya moyo wangu na ndiyo maana tumepata majibu haraka iwezekanavyo mwezi Januari mwaka huu”,aliongeza. 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko alisema “Ni wajibu wetu sasa kuhakisha kwamba,hizi pesa tulizopewa kwa ajili ya madarasa mawili na vyoo sita kwa kila shule,tuhakikishe hatuishii madarasa mawili pekee bali tujenge madarasa matatu,tuhakikishe tunaweka nguvu kazi zetu ikiwemo sisi wenyewe kuchimba misingi”. 

Hata hivyo wananchi walisema wapo tayari kuchangia nguvu kazi zao kwenye ujenzi wa madarasa na vyoo vya shule na ili kuonesha utayari walianzisha harambee kwenye mkutano ambapo shilingi 140,500 zilipatikana papo hapo,ahadi ya tripu 21 za mchanga, maji tripu 10 pamoja na mifuko 9 ya saruji.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Tinde na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeo - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Wakazi wa Tinde wakimsikiliza mbunge wao Azza Hilal.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza na wakazi wa Tinde.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza na wakazi wa Tinde.
Wakazi wa Tinde wakiwa kwenye mkutano.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akiwasisitiza wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akielezea kuhusu mchango wake wa mabati 23 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na Tinde B.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi mabati 23 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na Tinde B.
Mwananchi akitoa mchango wake wakati wa harambee iliyoanzishwa na wananchi kuchangia ujenzi wa vyoo vya shule na madarasa katika shule za Tinde A na B.
Mwenyekiti wa kijiji cha Jomu George Masele akionesha eneo ambapo panajengwa vyoo katika shule ya msingi Tinde B.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza wakati akikagua maeneo ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Tinde A na Tinde  B.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: