Pichani kulia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo akikabidhi baadhi ya vitu kwa mmoja wa akina mama mara baada kuwatembelea akina mama hao wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia (Delivery Pack) 350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa.
Baadhiya vifaa mbali mbali vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde kwa akina mama Waja wazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde na ujumbe wake akiwasili kwenye moja ya zahanati jijini Dodoma kukabidhi baadhi ya vitu kwa akina Mama wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia (Delivery Pack)350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa.
Pichani kulia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo akikabidhi baadhi ya vifaa mmoja wa akina mama mara baada kuwatembelea akina mama hao wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia*(Delivery Pack) 350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa.
Picha ya pamoja
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.
MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewatembelea wakina mama wajawazito katika vituo vya afya na zahanati katika Jiji la Dodoma na kutoa msaada wa vifaa vya kujifungulia.
Baadhi ya vifaa hivyo ni Delivery Pack 350 yenye thamani ya Sh.milioni saba, mashuka 100 yenye thamani ya Sh.milioni 1.1, pakiti 40 za dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Sh.milioni moja, na Carton 30 za Maji ya Kunywa ambapo msaada huo umesababisha uwepo wa furaha kubwa kwa wakina mama wajawazito na kushindwa kuficha hisia zao na kudondosha machozi ya furaha.
Akizungumza leo baada ya kukabidhi msaada huo Mavunde amesema ameamua kutumia siku ya leo ya Februari 14,2019 kuonesha upendo kwa wakina mama hao wa Dodoma kwa kusaidia vifaa hivyo muhimu wakati wa kujifungua na hiyo ni shukrani anayoirudisha kwa mama zake hao kutokana na upendo wao mkuu.
Akimshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada huo mkubwa,Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dk.Gatete Mahava amemuomba Mbunge Mavunde kuendelea kusaidiana na Serikali kutatua changamoto katika sekta ya Afya hasa katika kituo cha Afya cha Makole ambacho kimefanyiwa upanuzi mskubwa baada ya kukamilika ujenzi wa wodi ya wakina mama kupitia fedha kiasi cha Sh.milioni 500 zilizotolewa na Serikali ya Rais Magufuli katika Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya.
Katika tukio hilo Mavunde aliambatana na viongozi wa CCM Wilaya,Mbunge wa Viti Maalum Bura, madiwani wa Kata,Wasaniii na Mama Lishe wa Soko kuu Majengo
Toa Maoni Yako:
0 comments: