Meddie Kagere raia wa Rwanda,mshambuliaji mwenye uchu wa mabao na mtu muhimu kwa simba.Huyu ndiye mchezaji pekee wa Simba ambaye hadi sasa ameifungia Simba jumla ya magoli 25. Magoli 12 kwenye ligi kuu, magoli 6 kwenye michuano ya ligi ya mabingwa. Magoli 7 kwenye sport pesa na mapinduzi cup.Kwa sasa ndiye mshambuliaji anayetisha na anayeitendea haki ajira yake. Tofauti na baadhi ya wachezaji wengine wa kimataifa waliowahi kuichezea Simba. Kama vile Simon Serunkuma, Dan Serunkuma, Mavugo, Niyonzima nk.Hadi sasa thamani ya Kagere inazidi kupanda kila siku.Kama leo akiuzwa atauzwa kwa dau kubwa tofauti na alivyonunuliwa.
2. Kagere ana nguvu,yuko imara,haanguki ovyo ovyo.Kwenye mechi dhidi ya Yanga Shaibu alimsukuma matokeo Yeye ndiye alianguka.
2. Kagere ana mbio.Kagere ana uwezo wa kukimbia na mpira bila kupoteza na kuweza kufunga.Alifanya hivyo dhidi ya JS Soura.
3. Kagere si mwepesi kukata tamaa.Ana tabia ya kuufata mpira Hadi aridhike kuwa umetoka au kipa amedaka.Kumbuka dhidi ya mbabane pale Dar,kwa njia hiyo alifunga goli.Wengi wa wachezaji wana tabia ya kuuacha mpira utoke kirahisi hata Kama angeweza kuupata.
4.Kagere ana akili kubwa ya mpira.Anajua asimame wapi ili mpira umfikie na aweze kufunga.Anajua mahali pa kupiga ambapo kipa hawezi kudaka.Angalia namna alivyowafunga Yanga ni sawa alivyofunga Al Ahly.
5. Tofauti na baadhi ya washambuliaji wengine wa ndani na nje ya nchi, Kagere ana upekee.Kuna washambuliaji Wana namna moja tu ya kufunga.Wapo ni maridadi wa kusubiri waletewe mpira walipo ndipo wafunge kama Chirwa. Wapo wanaweza kufunga kwa vichwa tu kama Makambo kumbizana hawawezi.Wapo wanaoweza kusubiri ndani ya box au karibu ya box ndipo huweza kufunga. Kagere hayuko hivyo anaweza kujipozisheni popote. Anaweza kuuhemea mpira yaani kuutafuta na kutoa pasi Kisha kukaa mahali apewe pasi. Anaweza kukimbizana na mabeki kwa eneo refu na kuwashinda Kisha akafunga.
6. Kagere ana nidhamu ya uchezaji.Huwezi kumwona anagombezana na refa au wachezaji wa timu pinzani hata pale asitendewa haki.Inaonekana nidhamu hiyohiyo ndiyo anayo kwa kocha wakati wa maelekezo ya jinsi ya kucheza.
7. Kagere hana tabia za kizembezembe. Huwezi kumwona amekaa,anafunga viatu,anatoka kubadili viatu, analalamika ovyo ovyo n.k.
8. Kagere anaamini ktk vitendo zaidi vya uwanjani. Jambo hili ndilo linamfanya azidi kuuduwaza ulimwengu wa soka ndani na nje ya Tanzania.Kuna siku aliwahi kuhojiwa kuhusu uwezo wake,Yeye alijibu "mchezaji hatakiwi kuongea sana vitendo vyake uwanjani ndivyo huongea."
Uwezo mkubwa wa Kagere,juhudi zake,maelekezo ya Kochi pamoja na ushirikiano wa timu nzima ndivyo vinamfanya Kagere aiweke pazuri Simba katika ligi kuu Tanzania bara na katika ligi ya mabingwa Afrika.Upachikaji wake wa mabao unsmfanya awe mchezaji wa pekee hapa Tanzania na Afrika.Wachezaji wa kitanzania wanatakiwa kujifunza kwa Kagere.
Toa Maoni Yako:
0 comments: