Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye ( wa tatu kushoto) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakipewa maelezo na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Meing'ataki kuhusiana na bwawa lenye viboko wengi katika Hifadhi hiyo liitwalo Mwanambogo wakati wajumbe ya Kamati hiyo walipofanya ziara ya kutembelea kwa ajili ya kujionea mradi wa kukuza utalii kusini wa Regrow ulipofikia na namna unavyotekelezwa.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Constantine Kanyasu.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Meing'ataki ( wa kwanza kushoto)/akitoa Maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye, ( wa pili Julia) Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla ( wa kwanza kulia)pamoja na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto) kuhusu uwanja wa ndege unaotarajiwa kuboreshwa na utakuwa na urefu wa kilomita 2.2 unatekekelzwa kupitia Mradi wa kukuza utalii kwa upande wa kusini( Picha na Lusungu Helela- MNRT). (Picha na Lusungu Helela)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla ( wa nne kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi jana mara baada ya Kamati ya Bunge ya Kudumu,Ardhi, Maliasili na Utalii kuondoka katika Hifadhi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe.Nape Nnauye wakizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla pamoja na Mjumbe wa Kamati hiyo Dkt.Steven Kiruswa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye ( wa tatu kushoto) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakifurahia jambo mara baada ya kutembelea ziwa la viboko vinavyojulilika Bean a bears kama maelezo na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Meing'ataki kuhusiana na bwawa lenye viboko wengi katika Hifadhi hiyo liitwalo Mwanambogo wakati wajumbe ya Kamati hiyo walipofanya ziara ya kutembelea kwa ajili ya kujionea mradi wa kukuza utalii kusini wa Regrow ulipofikia na namna unavyotekelezwa.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Constantine Kanyasu.
---
Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii imeishauri Serikali imalize mazungumzo na Benki ya Dunia juu ya hatma ya mkopo wa mradi wa kukuza utalii kwa upande wa kusini baada ya Benki hiyo kuonesha kusuasua kufuatia Serikali ya Tanzania kusimamia uamuzi wake wa kuanzisha Mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji.
Hatua hiyo inakuja baada ya serikali ya Tanzania kukopa jumla shilingi bilioni 345 kutoka Benki ya Dunia ili kukuza utalii katika maeneo ya Kusini kupitia mradi ujulikanao kama Resilient Natural Resource Management for Tourism Growth ( REGROW)
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti Kamati hiyo, Mhe .Nape Nnauye baada ya Kamati hiyo kufanya ziara katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiwa ni moja ya ziara ya kutembelea ukanda wa kusini kwa ajili ya kuona mkopo huo umefikia wapi na namna mradi huo unavyotekelezwa.
Amesema uamuzi huo wa Serikali wa kutaka kufungua Utalii wa Kusini ni wa muhimu sana hata endapo mazungumzo hayo yanayoendelea yatakwama Serikali ifikirie mbadala wake lengo likiwa ni kuongeza mapato yatokanayo na utalii.
Katika mradi huo Hifadhi za Mikumi, Ruaha, Udzungwa pamoja na Pori la Akiba la Selous zinatarajiwa kunufaika kupitia mkopo huo lengo likiwa ni kufanya ukanda wa kusini kuwa lango la Utalii kama ilivyo kwa ukanda wa kaskazini.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo ameishauri Serikali kuwa endapo fedha za mkopo huo zitapatikana iandae utaratibu wa kuufanya mradi huo uwe wa kibiashara badala ya ilivyo sasa ambapo kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha hizo yamejikita katika uhifadhi zaidi.
Amesema fedha inayowekezwa ni nyingi na italipwa na watanzania sasa ni vizuri itakapowekezwa itoe matokeo yaliyokusudiwa ambayo yatafanana na thamani ya mkopo wenyewe.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla amesema kumekuwa na mashaka kidogo kutoka kwa Wafadhili ambao wanatukopesha pesa hizo baada ya kuona mradi wa kufua umeme katika mto Rufiji unatekelezwa.
Amefafanua kuwa Wafadhili hao wanahofu kuwa kutakuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira na hivyo mradi wa Regrow utashindwa kutekelezwa kwa vile kivutio katika Pori la Akiba la Selous kitabadilika sura yake
Ameelezea kuwa Serikali imefanya jitihada za kuhakikisha kuwa mazingira ndani ya Pori hilo hayataharibiwi na hivyo mradi wa Regrow unaweza ukaendelea kama ilivyopangwa.
Amesema moja ya hatua zilizochukuliwa na serikali ni kuvihamisha viumbe ambavyo vilikuwepo katika eneo linapotarajiwa bwawa kujengwa, Hivyo viumbe hao wataendelea kuwepo na wanaweza kurudi katika eneo lao la awali.
Aidha,Mhe.Kigwangalla amesema hata kama itatokea viumbe hao wakapotea kutokana na ujenzi wa bwawa hilo basi viumbe na mimea iliyokuwepo katika eneo hilo vitarudishiwa kwa sababu tayari imechukuliwa na kuhifadhiwa kwenye maabara ya vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo hapa nchini kikiwemo Chuo kikuu Cha Dar es Salaam pamoja na Sokoine.
"Tumewaeleza kuwa mashaka yao hayawezi kuzuia huu mradi na bila shaka wametuelewa hivyo tunasubilia uamuzi wa mwisho wa kuamua wanatukopesha au hawatukopeshi" amesema Mhe.Kigwangalla.
Pia amesema katika mradi huo yatachimbwa mabwawa makubwa matatu ambayo yatatumika kama vyanzo vya maji kwa wanyama waliopo katika bonde la Mto Rufiji
Akizungumzia manufaa ya mkopo huo , Waziri Kigwangalla amesema utatumika kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara pamoja na viwanja vya ndege ambavyo vitakuwa vichocheo vikubwa katika kukuza na kuendekeza utalii kwa ukanda wa kusini.
Toa Maoni Yako:
0 comments: