Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kimefanyika leo Disemba 4, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumzia agenda za kikao, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Bw.John Magale Shibuda amesema kuwa kikao hicho kitakuwa na ajenda ya kujadili muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2018 na uchaguzi wa Viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa.
Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa inaundwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa kamati nne za Baraza la Vyama vya Siasa.Naibu Msajili wa vyama vya Siasa (kushoto ) akipokea Nakala ya Maelezo ya Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa yenye ushauri wa jinsi ya kuunda siasa adilifu na bora za kujenga ustawi na maendeleo ya jamii, uchumi na Taifa iliyowasilishwa kwa Waziri Mkuu , Mhe. Kassim Majaliwa mapema mwaka huu kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Bw.John Magale Shibuda.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Bw. Abdalah Juma Saadalla .
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Bw.John Magale Shibuda afafanua jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kimefanyika leo Disemba 4, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. Kulia kwake ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Ohammed Ali Ahmed na kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Bw. Abdalah Juma Saadalla
Kikao kikiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments: