Waziri wa Madini Angela Kairuki Akikata Utepe Kuzindua Kitabu Cha Simulizi ya za Lukundo Kilichoandikwa na Mama Fatma Kange, Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Same Rose Staki Pamoja na Salehe Njaa mume wa Mwaandishi wa kitabu hicho (Kushoto).Uzindui Huo Umefanyika Jijini Dar es salaam.Aidha Waziri Kairuki Amewataka Watanzania Kupenda vitu vya Nyumbani ili kuwapa Moyo watazania wenzetu katika Kazi nao na Ubunifu wao.Amepongeza Sana Mwandishi wa Kitabu Hiko Bi Fatma Kange ambaye katika Kitabu hicho amegusia Maisha na Malezi ya Kabila la Wapare.
Fatuma A. Kange, amefurahi kuzindua kazi yake kubwa “ KITABU CHA SIMULIZI ZA LUKUNDO” ambachoamekifanyia utafiti na kuelezea mambo mengi ya msingi kwa muda mrefu mno.. imemchukua takribanimiaka 10 kukamlisha kazi yake hiii kuntu! wakati wa ufunguzi Fatuma alisema amekuwa akitumia likizoyake kila mwaka anapokwenda kijijini kwao Makanya,Kimunyu Same kufanya utafiti. anasema alikuwaanaona raha kwenda kwao, kumsalimia babu yake Mzee Juma Kimomwe na bibi yake Kozaina naKorashid ambao kupita likizo hiyo, alijikita kufanya tafiti ndogondo za kitongoji cha kimunyu ambachoamelelewa na kutumia muda huo vizuri kuhifdha habari mbalimbali. maeneo aliyoyataja ni yale yoteambayo yanaizunguka kitongoji cha kimunyu kama yote ya Chome, Mwembe, Hekapombe,Mongoloma,Mnazi, Mzumura, Tae, Makuyuni, Makanya stasheni, Mgwasi na kimunyu.
Uzinduzi ulipata wafadhili wakutosha na kushukuru kwamba kazi aliyoifanya kumbe imekuwa ya faida!kitabu chake kimechambuliwa na maprofesa waliobobea katika kiswahili na kukipa kitabu hicho nguvuya kuthibitishwa na Mhe. mama Samia Suluhu Hassan-Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, ambaye amekipa heshima kubwa ya kukiandikia dibaji. Fatuma Kange amejionamwenye bahati kubwa sana.kikubwa katika kitabu hicho, Fatuma ameeleza masuala ya malezi kwa mtizamo wa kipare, dhana zakipare zote zililenga kumjenga mtoto wa kike, hivyo amezungumzia, kuratera, kuja ghwi, kirighi cha ngwina upendo kama ambavyo bibi yake Kozaina alimpa! mapenzi makubwa yaliyotukuka! hakuna kama bibi kozaina na ndiyo maana ameona ahifadhi kumbukumbu zote alizolelewa na bibi yake katika kitabu hikikikubwa cha SIMULIZI ZA LUKUNDO. ambacho kimebeba jina la kozaina.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: