Afisa Tarafa Pangani Mjini Bi. Zuhura Abdulrahmani wa pili kulia akiwa kwenye kikosi hicho leo amekutana na kufanya kikao na kamati ya awali kwa ajili kuanzisha Jogging Club ya
Pangani mjini.
Afisa Tarafa Pangani Mjini Bi. Zuhura Abdulrahmani wa tatu kutoka kushoto aliyevaa kilemba akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau hao mara baada ya kumaliza kikao hicho leo kwa ajili ya kuanzisha Jogging Club ya Pangani mjini wa tatu kutoka kushoto ni Mohamed Hamie kutoka Pangani FM
Afisa Tarafa Pangani Mjini Bi. Zuhura Abdulrahmani leo amekutana na kufanya kikao na kamati ya awali kwa ajili kuanzisha Jogging Club ya Pangani mjini.
.
Lengo la kuanzishwa jogging Club hiyo ambayo itakuwa ni ya kwanza Pangani Mjini ni kuhamasisha mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya, kwa mustakabali wa maendeleo ya Pangani.
.
Kamati hiyo ambayo imejumuisha takribani wajumbe 13, imefanya kikao chake cha kwanza katika ukumbi wa halmashauri wa wilaya, ambapo mbali na kuwa na lengo kuu pia ilikubaliana kuwa na malengo mengine madogo madogo.
.
Malengo hayo ni pamoja na kushiriki katika shughuli za kijamii, kuunganisha vijana pamoja na kubadilishana mawazo, pia kusukuma ajenda mbalimbali za kimaendeleo za serikali.
.
Bi Zuhura ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, amepokea mapendekezo kadhaa ya uanzishwaji wa jogging hiyo kuwa ni pamoja na vifaa vya mazoezi ikiwepo mipira, jezi, muziki, pamoja na mkufunzi.
.
Jogging Club hiyo ambayo imepewa jina la PANGANI JOGGING CLUB inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni punde baada ya kukamilisha utaratibu wa usajili.
Toa Maoni Yako:
0 comments: