Mshindi wa nyumba na sh Milioni 20 wa Biko, Alex Nyoka, mkazi wa Mbalari mkoani Mbeya, akiwa na furaha tele baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mkoani Mbeya.
Mshindi wa nyumba na sh Milioni 20 wa Biko, Alex Nyoka, mkazi wa Mbalari mkoani Mbeya, akiwa na furaha tele baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mkoani Mbeya. Kulia kwake ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.

Na Mwandishi Wetu, Mbeya.

Mshindi wa pili wa nyumba na sh Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko, Alex Nyoka, amekabidhiwa fedha zake jana mkoani Mbeya, ikiwa ni siku moja baada ya kuibuka kidedea kutoka kwenye droo ya 158 ya Biko, iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana Lujewa, Mbalari mkoani Mbeya na kuongozwa na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, huku mshindi huyo akizungumzia mkakati wake wa kujikwamua kimaisha baada ya kuibuka mshindi wa Biko.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Nyoka ambaye ni dreva wa tax, alisema amechelewa kuamini kama ni kweli anaweza kuwa mshindi wa fedha nyingi na nyumba kutoka kwenye bahati nasibu pendwa ya Biko nchini Tanzania.

"Bado siamini kama ni kweli nimeshinda bahati nasibu ya Biko, ingawa nimeshika fedha hizi kwa sababu nilikuwa natamani nishinde ingawa najua waliokuwa wanataka ushindi huu sipo peke yangu.

"Kwakweli namshukuru Mungu kwa zawadi hii kubwa, huku nikiwataka Watanzania wengine wacheze Biko ili washinde kwa sababu sijawahi kuona bahati nasibu inayochezeshwa kwa uwazi na hata fedha zinaingizwa bank moja kwa moja, hivyo hakuna dalili ya unganyifu," Alisema.

Naye Grace Kaijage, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, alisema wimbi la mamilionea na wamiliki wapya wa nyumba linaendelea, huku akisema popote atakapoibuka mshindi wa nyumba atapata fedha na nyumba yake, akisema wanaoshirikiana nao Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wana miradi ya nyumba katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

"Tumekuja Mbeya kumkabidhi mshindi wetu fedha zake ambapo jana tulimkabidhi fedha, lakini pia hatuondoki hadi leo apewe nyumba yake kutoka NHC ambayo hununuliwa na Biko kwa ajili ya washindi wetu popote walipo, hivyo naomba waendelee kucheza Biko ili waibuke mamilionea na wamiliki wapya wa nyumba kutoka Biko," Alisema.

Grace alisema zawadi za papo kwa hapo za Biko kuanzia sh 5,000, 10,000, 20,000 hadi sh Milioni moja zinaendelea kutolewa kwa kupitia Biko inayochezwa kwa kufanya miamala kwenye simu za mikononi ya Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money kuanzia sh 1,000 na kuendelea, namba yao ya Kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

Droo kubwa huchezeshwa kila Jumatano na Jumapili, huku kuanzia Jumatano na Jumapili, watanzania wanaocheza Biko wakitarajiwa kushinda nyumba na sh Milioni 20.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: