Mtaalam wa Mambo ya Hedhi Salama Bw. Sylvester akitoa somo kwa upana juu ya maswala ya Hedhi salama na namna gani wanawake wanaweza kujipatia msaada zaidi wakati wakiwa katika hali hiyo.
 Baadhi akina mama, wakina dada na mabinti wakiwa katika chakula cha usiku na kusikiliza mambo mazuri yaliyo andaliwa na wataalam mbalimbali.
Mtaalam wa Mambo ya Saikolojia na Magonjwa ya akili Dkt. Hariel Mfagavo akielezea umuhimu wa wazazi kuwalea watoto wao kwa weredi mkubwa tangia wakiwa watoto, pia alizungumzia namna ukatili wa kijinsia unavyoweza kukatisha ndoto za watu na vile vile unavyoweza kuharibu maisha ya wahanga wengi na kuwasihi wazazi wasipende kuwalea watoto kwa kuwanyanyasa.
Baadhi ya waliohudhulia 'Dodoma Ladies Out' wakiwa katika tukio hilo
Mtumishi wa Mungu akitoa somo la uhusiano wa imani zetu pamoja na kumshirikisha Mungu katika mambo yetu mbalimbali ili tuweze fanikiwa, pia hofu ya Mungu hasa tunapofanya vitendo ambavyo havimpendezi, na kuwasisitiza wazazi na walezi kuwapenda watoto.
 Kulia ni MC wa  Shughuli hiyo Nancy akiendelea kusherehesha 
Mmoja wa akina Mama akiwafunda akina mama wenzake, akina dada na mabinti namna ya kuishi vema katika jamii na kumtanguliza Mungu katika mambo yao, na kusisitiza kuwa mama anajukumu kubwa la kulea watoto  na kuwatunza vema kwa usaidizi wa baba.
Hii ndio kamati iliyo andaa tukio zima la Dodoma Ladies Out
Picha ya pamoja ya wote waliohudhulia katika hafla hiyo iliyowakutanisha akina mama, akina dada na mabinti Jijini Dodoma. (Picha zote na Fredy Njeje).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: