Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhusu historia ya maisha yake pamoja na uanzishwaji wa Taasisi ya Dkt Kikwete katika hafla ya iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inmi Patterson akitoa shukrani kwa mchango pamoja na mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Marekani katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka MMG).
Sehemu ya wandau mbalimbali wa maendeleo wakiwa katika hafla hiyo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwanzilishi wa Taasisi ya Jakaya Kikwete Dkt. Jakaya Kikwete(kulia) akionyeshwa moja ya Picha na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Marekani hapa nchini (AMCHAM) Garry Friend (kushoto) iliyotoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ikiashiria kutambua mchango wa Serikali ya Tanzania.


Na Mwandishi Wetu.

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwanzilishi wa Taasisi ya Jakaya Kikwete Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa taasisi yake pamoja na kitabu chake cha The Journey Of My Life alifikiria kuanzisha vitu ambavyo vitakuwa kumbukizi  kabla ya kumaliza uongozi wake akiwa kama Rais.


Dkt. Kikwete ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla maalum ya Chakula cha jioni iliyoandaliwa na Chemba ya Biashara ya Marekani hapa nchini (AMCHAM) kwa lengo yakuishukuru Serikali ya Tanzania.

Amesema katika uongozi wake marafiki walifikiri jambo ambalo atalifanya mara baada ya kumaliza utumishi wa umma aliohudumu kwa miaka 40, ambapo alitaka kuweka uzoefu na mawazo yake katika maandishi ili yasiweze kufutika.

Kikwete amesema katika kitabu cha The Journey of My Life ameeleza kuhusiana na taasisi ya Jakaya na maisha yake tangu akiwa mdogo huko kijijini Msoga pamoja na uzoefu wa uongozi kwa miaka 40.

Dkt. Kikwete amesema katika kitabu chake amegusia maeneo mbalimbali yakiwemo kilimo, afya, vijana na utawala.

Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inmi Patterson amempongeza Dkt. Kikwete kwa uthubutu na amewashukuru watanzania kwa ukarimu, upendo na ushirikiano pamoja na kutunza amani hapa nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: