WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako akizungumza katika kongamano la Wadau wa elimu wilayani Pangani ambalo lilikwenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni shule ya Sekondari Mwera kulia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM0 kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah halfa iliyofanyika mjini Pangani
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako
Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza katika kongamano hilo kulia ni WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza katika kongamano hilo.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako kulia akitoka kukagua mabweni ya moja ya shule ya Sekondari wilayani Pangani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani nyuma ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako wa pili kutoka kushoto akiwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wakirufahia jambo wakiwa kwenye kivuko wakielekea ng'ambo ya pili ya mto Pangani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako akishuka kwenye kivuko akiwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto na Mkuu wa wilaya ya Pa ngani Zainabu Abdallah.
---
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako amesema kwamba wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma kwa kipindi cha miaka saba kama ilivyokuwa awali.
Proffesa Ndalichako aliyasema hayo mjini Pangani wakati wa Kongamano la Elimu wilayani Pangani lililoenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzoi shule ya sekondari Mwera mbapo alisema suala la muda wa elimu msingi lipo kwa mujibu wa sheria ya elimu ya mwaka 1982.
Alisema sheria hiyo imeweka bayana kwamba muda wa elimu ya msingi ni miaka saba na bado sheria hiyo haijafanyiwa marekebisho hivyo wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma miaka saba.
Akitolea ufafanuzi suala hilo alisema ikifika mahali kama kutakuwa na ulazima wa kubadilisha miaka ya kwenda shule kitakachotanguliwa ni kufanya marekebisho ya sheria kwa sababu jambo linalokuwa ndani ya sheria huwezi kulifanyia mabadiliko bila kuanza kufanya marekebishi ya sheria husika.
“Niwatoe hofu watanzania kwamba suala la kisheria huwezi kubadilika kwa tamko wala waraka wa kamishna wa elimu au kubadilika kwa maelekezo mengine yoyote bali linaweza kubadilika pale sheria ya elimu 1982 kwenye kipengine kinachoeleza muda wa elimu ya msingi miaka 7 kitakapofanyiwa marekebisho”Alisema Waziri Proffesa Ndalichako
Alisema baada ya kufanyiwa marekebisho ndio inaweza kubadilika na haitakuwa kinyumenyume na itaweka bayana kwa sababu badiliko kama hilo ni kubwa la sera na kisheria hivyo watu watafahamu mapema.
“Kumekuwa na mchanganyika kwa sababu sera ya elimu ya mwaka 2014 imeonyesha serikali itakuja kuweka utaratibu lakini haikusema itaweka lini kwamba elimu ya msingi iwe lazima mpaka sekondari”Alisema.
Alisema bado hatujawa tayari kuwa elimu ya msingi na sekondari kwa wanafunzi wote hivyo tunaendelea kuboresha elimu ya msingi na sekondari kuhakikisha mazingira mzuri ya kufundisha na walimu wa kutosha.
Alisema watakapoona wamefika mahali na kuona haja ya kufanya hayo watu wamekuwa wakiulizia serikali itawashirikisha wadau wote kwamba tunakwendaje huku akieleza mkakati ni serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa alimueleza Waziri huyo kwamba namna walivyohamasisha suala la elimu wilayani humo ili kuwapa uelewa wananchi juu ya umuhimu wa elimu ikiwemo kutoa wimbo wa kuhamasisha.
“Mh Waziri kutokana na awali kuwa na hali ambayo sio nzuri kwa elimu wilayani hapa mimi na Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso tulikwenda studio kurekodi nyimbo ya kuhamasisha elimu tunashukuru Mungu hali imebadilika na suala la elimu limekuwa likipewa kipaumbele”Alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments: