Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mradi wa uchakataji majitaka Toangoma, Temeke jijini Dar es Salaam uliojengwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) na Shirika Shirika la PDF chini ya Shirika la Water Aid TanzaniaKushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbagala Ally Mangungu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso (katikati mwenye shati jeupe) akizundua mradi wa uchakataji majitaka Toangoma, Temeke jijini Dar es Salaam uliojengwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) na Shirika Shirika la PDF chini ya Shirika la Water Aid Tanzania.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akipata maelekezo ya mradi wa kuchakata maji taka toka kwa Mhandisi Elias Kazingoma kutoka Shirika la PDF. Mradi mzima wa kuchakata majitaka umejengwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) na Shirika la PDF chini ya Shirika la Maji la Water Aid.
Mhandisi Elias Kazingoma kutoka Shirika la PDF (Kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso moja ya sehemu inayotumika kuhifadhia majitaka kwenye mradi wa Uchakataji majitaka wa Toangoma.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amezindua mradi wa uchakataji majitaka uliopo eneo la Toangoma Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mradi huo uliotekelezwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) na Shirika la PDF chini ya Shirika la Water Aid Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo Aweso ukiwa na vipengele vikuu vinne ambavyo ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma za uhifadhi na udhibiti wa taka ngumu kwa wakazi wa kata 23 za Manispaa ya Temeke.
Mradi wa Tuangoma umetumia kiasi cha Milioni 359 ukijumuisha ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali ambayo ni pamoja na sehemu ya Kuchujia taka ngumu (screening chamber), tenki la kuhifadhia majitaka kwa muda mrefu (balancing Tank), mtungi wa kuchakata majitaka na kutengeneza gesi (biogas Dome) sehemu ya kuchujia majitaka (perforated grave filter) na sehemu ya kukaushia tope la majitaka.
Mtambo huo una uwezo wa kuhifadhi majitaka kiasi cha lita elfu hamsini (50m3) na uwezo wa kuhudumia wananchi 93,000 na uwezo wa kuzalisha gesi kiasi cha lita 4000 kwa siku ambayo inaweza kuhudumia takribani kaya 250 kwa mwezi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani hususani kupikia.
Toa Maoni Yako:
0 comments: