Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kilimampimbi iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao.
Baadhi ya wanafunzi wa Vwawa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Vwawa iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la kuongeza mapato yatokanayo na utalii Npamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na walimu wa shule ya sekondari ya Vwawa iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi wa shuke hiyo kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilolo iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi, Bi. Hossana Mshule wakati wakielekea kukagua baadhi ya majengo yaliyojengwa kwa mfuko wa jimbo la Vwawa.
NA LUSUNGU HELELA- SONGWE
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ameanza ziara ya kimkakati ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini lengo likiwa ni kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao kwa wanafunzi hao.
Mhe. Hasunga amesema sekta ya utalii inaweza kuongeza pato lake maradufu iwapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wataanza kujua umuhimu juu ya utalii wa ndani bado angali wakiwa wadogo.
Katika ziara hiyo aliyoianza mkoani Songwe wilayani Mbozi, Naibu Waziri Mhe. Hasunga ameweza kutembelea shule za Sekondari tatu ikiwemo Shule ya Kilimampimbi, Vwawa pamoja na Ilolo ambapo amezungumza na wanafunzi pamoja na walimu kuhusu umuhimu wa utalii wa ndani.
Amefafanua kuwa Wanafunzi ni mabalozi wakubwa wa mabadiliko, wanapopata elimu juu ya utalii wa ndani wataweza kuifikisha kwa wazazi, walezi pamoja na jamii kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Mhe. Hasunga ametoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliokuwa wakijibu maswali kuhusiana na vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Amesema sekta ya utalii inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na inaweza ikawa asilimia 30 kama kutajengeka utamaduni kwa jamii wakiwa bado wanafunzi kuhusu umuhimu wa kutenga muda pamoja na pesa kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
‘’Nchi yetu imejaliwa kuwa na vivutio vingi lakini imekuwa haifanyi vizuri ukilinganisha na nchi kama Misri aambao wao hawana vivutio vingi kama tulivyonavyo sisi, Wenzetu wana magofu pekee lakini wametuacha mbali’’ amesema Mhe. Hasunga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: