Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Wazee waishio Makao ya Wazee Sukumahela Wilayani Manyoni wakati wa ziara take inayoendelea Mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Jiko kinapoandaliwa chakula cha Wazee waishio Makao ya Wazee Sukumahela Wilayani Manyoni wakati wa ziara take inayoendelea Mkoani Singida.
Na Anthony Ishengoma.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida kuhakikisha wazee wasiojiweza wanaoishi Makao ya Wazee ya Taifa Sukamahela wanapatiwa vyandarua kwa ajili ya kujikinga na Malaria.
Naibu Waziri Ndugulile ametoa agizo hilo alipotembelea makao hayo yaliyoko nje kidogo ya mji mdogo wa Manyoni kujionea hali halisi ya maisha ya Wazee wasiojiweza.
Dkt. Ndugulile ametoa muda wa wiki mbili kwa Mganga Mkuu Mkoa kutekeleza jambo hilo na kutaka mrejesho wa utekelezaji wa agizo hilo.“Hili ni kosa ambalo siwezi kulisamehe tuna vyandarua vingi vya kutosha sioni sababu wazee hawa kulala kwenye vyumba bila vyandarua, nawapa wiki mbili kuhakikisha kila mzee analala kwenye chandarua.,” Aliagiza Dkt.Ndugulile.
Pia Dkt. Ndugulile amewataka watendaji wa Idara ya Afya wa Zahanati ya Sukamahela iliyopo katika eneo la makao ya Wazee hao kuhakikisha wanakuwa na dawa za kutosha hasa zile maalumu kwa ajili magonjwa ya Wazee.Makao ya Wazee Sukamahela pamoja na mambo mengine yanayowakabili na upungufu wa chakula, na wamekili kuchoshwa na ulaji wa aina moja ya mboga hivyo kutoa ombi lao kwa Naibu Waziri kutatua changamoto hiyo.
Naibu Waziri Ndugulile amehaidi kushughulikia suala la ukarabati wa majengo chakavu ya yaliyopo katika Makazi hayo.Kwa nyakati tofauti wazee waishio katika makazi hayo wamelalamikia ukosefu wa umeme katika makazi hayo, dawa za magonjwa ya ukoma na vifaa vidogo vidogo kwa ajili ya usafi na kilimo cha mbogamboga pamoja na miundo mbinu chakavu ya vyoo.Aidha Dkt.Ndugulile amesema serikali inakusudia kufunga baadhi ya vituo na kuvipanga kikanda ili iweze kudumisha huduma kwa wazee wasiojiweza lakini kugeuza makazi yatakayofungwa kuwa nyumba salama kwa ajili kupambana na vitendo vya kikatili.
Naibu Waziri Ndugulile yupo mkoani Singida kufuatilia utekelezaji wa masuala ya Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments: