*Mradi wa HAKI YETU wakutana na Maafisa Maendeleo na ustawi wa jamii Kigoma na kuzungumza madhara ya kuwatenga watu wenye ualbino

*Maafisa Maendeleo ya Jamii, na ustawi wa jamii Kigoma wapigwa msasa uelewa kuhusu Ualbino

Maafisa Maendeleo ya Jamii, na ustawi wa jamii, kutoka manispaa ya kigoma Ujiji leo wamehudhuria mafunzo ya uelewa kuhusu ualbino na elimu ya Amani na maadili iliyotolewa na mradi wa Haki Yetu mkoani Kigoma.

Mradi huu huu umekua ukiendeshwa tokea mwezi Aprili mwaka huu katika Mikoa ya kigoma na maeneo ya jirani kwa ushirika wa wadau Mbalimbali lengo lao likiwa ni kutoa msaada kwa jamii kuelewa zaidi kuhusu ualbino, kupunguza imani potofu, kuwajengea watu wenye ualbino misingi ya kujiamini ualbino pamoja na kutengeneza jamii shirikishi isiyokuwa na ma waa ya ubaguzi wa aina yoyote kwa watu wenye ualbini

Katika mradi huu misingi muhimu ambayo imekua ikiwekewa msisitizo ni pamoja na kuzingatia utu, kuwapa nafasi watu wenye ualbino bila kuwabagua, kushirikiana nao kwenye maswala ya elimu na uchumi lengo likiwa ni kujenga Taifa bora.

Mradi wa Haki Yetu unatekelezwa na Mashirika ya Under The Same Sun, CEFA Tanzania na GNRC Tanzania, ukilenga kuelimisha jamii kuhusiana na ualbino.
Viongozi wakiendelea kutoa somo la Ualbino.
Wadau wakifuatilia somo.
Picha ya Pamoja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: