Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (mwenye shati nyeupe) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami ya Mkuranga – Kisiju, mkoani Pwani
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyevaa shati nyeupe) akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kushoto) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami ya Mkuranga – Kisiju wakati wa ziara yake mkoani Pwani
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa kwanza kulia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami ya Mkuranga – Kisiju wakati wa ziara yake mkoani Pwani
Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Wambura (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami ya Mkuranga – Kisiju mkoani Pwani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami ya Mkuranga – Kisiju wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Pwani

Mhe. Suluhu amefanya ziara yake hiyo ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami ya Mkuranga – Kisiju iliyopo kwenye Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani

Suluhu amesema kuwa Tanzania ni lango la kuingia Afrika ndio maana Serikali tumechukua jukumu la kujenga miundombinu mbali mbali ya barabara, anga, reli, bandari na mingine ili kuhakikisha kuwa tunakuza uchumi wa taifa letu na kutumia fursa hii kufikia uchumi wa kati kwa kuzingatia kuwa mkoa wa Pwani unaongoza kwa kuwa na uwekezaji wa viwanda vikubwa, vya kati na vidogo vipatavyo jumla ya viwanda 429 vya wawekezaji wa kutoka ndani na nje ya nchi ambapo miundombinu ya barabara ni muhimu katika kuharakisha na kuwezesha ujenzi na ukuaji wa viwanda nchini

Akiwa kwenye ziara hiyo, ametembelea na kukagua barabara hiyo na kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo ya kutoka Mkuranga hadi Kisiju yenye urefu wa jumla ya kilomita 45.77 ambapo hadi sasa kipande chenye urefu wa barabara yenye kimomita 1.84 imejengwa kwa kiwango cha lami

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa katika ziara hiyo, amemweleza Mhe. Samia kuwa kilomita 1.84 ya barabara ya Mkuranga – Kisiju imejengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi bilioni 1.850. Nditiye amesema kuwa Wizara itahahakikisha kuwa inafanya za kutatua kero mbali mbali za wananchi na kuhakikisha kuwa Serikali inajenga na kuboresha miundombinu ya barabara ili kuleta maendeleo kwa wananchi

Naye Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuanza ujenzi wa barabara ya Mkuranga hadi Kisiju kwa kuwa jambo hili lilikuwa ni mfupa mgumu ila ameuweza. “Barabara ya Mkuranga – Kisiju ni barabara kuu inayotuunganisha na mikoa ya jirani, inahudumia kata saba na watu zaidi ya 40,000” amesema Ulega. 

Pia amefafanua kuwa barabara ya Mkuranga – Kisiju ni barabara ya kiuchumi, yenye kubeba korosho, inapita eneo la uwekezaji wa viwanda, linapita bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara. “Barabara hii ni kilio chetu, tunatamani sana barabara hii ikamilike”, amesema Ulega.

Naye Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Wambura amesema kuwa mkataba wa ujenzi wa barabara ya Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 1.84 na yenye gharama ya shilingi bilioni 1.850 umeanza kutekelezwa mwezi Februari 2018 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari mwaka 2019 na inajengwa na mkandarasi Kings Builders (T) Ltd na kusimamiwa na Kitengo cha TECU (TANROADS Engineering Consulting Unit), TANROADS ambapo mradi huu utajumuisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami pamoja na mitaro ya maji

Wambura ameongeza kuwa barabara ya Mkuranga – Kisiju ina urefu wa kilomita 45.77 ambayo inaunganisha Wilaya ya Mkuranga na Wilaya ya Mafia zilizopo mkoani Pwani na inaungana na barabara kuu inayokwenda mikoa ya kusini. Pia, amesema kuwa barabara ya Mkuranga – Kisiju ni kiungo muhimu cha usafirishaji kati ya bandari ya Kisiju na kisiwa cha Mafia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: