Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd,Mohamed Kiluwa ( wa nne kulia) pamoja na ujumbe wake wakiwa na wageni wao katika picha ya pamoja kwenye moja ya chumba maalum cha kufikia Wageni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,mara baada ya kuwasili Oktoba 27,2018 jijini Dar kutoka nchini China .Kampuni hiyo yenye ujumbe wa watu wa Watano umekuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Kiluwa Group Ltd kufanya mazungumzo mbalimbali yakiwemo ya kutafuta fursa za uwekezaji ikiwemo pia kuonana na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC).
Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd, Mohamed Kiluwa pamoja akipokea zawadi aliyoletewa na mgeni wake,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong mara kwenye moja ya chumba maalum cha kufikia Wageni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,mara baada ya kuwasili Oktoba 27,2018 kutoka nchini China.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd, Mohamed Kiluwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong wakimsikiliza Meneja wa kampuni ya Kiluwa Group Ndugu Madoweka (ambaye ni mkalimani wa lugha ya Kichina), akifafanua jambo kurahisisha mawasiliano kwa mgeni wao Ndugu Mayi Hong akiwa ameambatana na ujumbe wake wa watu wanne kutoka kwenye kampuni yake ambayo inajishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa za ngozi nchini China.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group, Naima Kiluwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar Oktoba 27,2018.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group, Naima Kiluwa pichani kati akiwa ameambatana na Wageni wake mara baada ya kuwapokea jana uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea nchini Chaina,Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendani wa kampuni ya Yinengda New Material Technology,Mayi Hong.kampuni hiyo inajishughulisha na uzalishaji/utengenezaji wa bidhaa za ngozi nchini China.
Toa Maoni Yako:
0 comments: