Washiriki wakifuatilia semina kwa umakini.
Katika kuendelea kusimamia haki na usawa kwa watoto wakike na makundi yaliyopo pembezoni, TGNP Mtandao kupitia semina zake za Jinsia na Maendeleo(GDSS) wanakukaribisha mkazi wa jiji la Dar es salaam na maeneo ya karibu katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani pamoja na miaka 25 ya shirika hilo.
Maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwaka duniani kote kila ifikapo tarehe 11 ya mwezi oktoba yenye lengo la kumpongeza na kuangalia changamoto mbalimbali zinazomfanya mtoto wa kike kushindwa kufikia malengo yake na kuzitafutia ufumbuzi na kwa upande wa GDSS watafanya maadhimisho hayo siku ya tarehe 10 ya mwezi huu wa kumi.
Muwezeshaji wa Semina Bw. Busungu Mathias akitoa ufafanuzi wa jambo katika semina ya GDSS wiki hii.
Akiongea katika semina ya GDSS mapema wiki hii Bw. Busungu Mathias kutoka TGNP Mtandao alisema kuwa shirika hilo linatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake na kuunganishwa na maadhimisho makubwa ya siku ya Mtoto wa kike duniani itapofika tarehe 13 ya mwezi huu wa kumi.
Aliendelea kusema kuwa katika maadhimisho hayo yatafanyika mambo mbalimbali kama Mashairi, Maigizo, Nyimbo, Ngonjera na vitu vingine vingi, huku wakijaribu kujitathmini kwa miaka hii yote 25 wamefikia wapi katika harakati za ukombozi wa wanawake na makundi yaliyopo pembezoni na kuweka mikakati mipya kwa kipindi kijacho.
Washiriki wa semina wakiwa katika kazi ya vikundi mapema wiki hii.
Ikumbukwe kuwa aliyesimamia kidete kuwepo kwa siku hii duniani ni Rona Ambrose ambye ni raia wa nchi ya Kanada, alichukua uamuzi huu baada ya kuona mtoto wa kike amechanganywa katika makundi mbalimbali na kashindwa kupewa siku yake mwenyewe, ndipo alipopeleka ombi katika Umoja wa Mataifa na ukawa ni mwanzo wa kuwepo kwa siku hii.
Na kwa upande wa Tanzania shirika la Plan International lilisimama ipasavyo kuhakikisha siku hii inatambulika kitaifa na inaadhimishwa kila mwaka ifikapo octoba 11, hivyo nchi yetu kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa na ilikubali kusaini mikataba ya kimataifa na kikanda ya kulinda haki za watoto na wanawake ilikubali kupitisha siku hii kuadhimishwa ndani ya nchi yetu.
Semina ikiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments: