Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shughuli ya harambee, Magreth Sitta akizungumza wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa maandalizi ya shuguli ya harambee ya wabunge, Profesa Anna Tibaijuka akizungumza wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda na Makamu Mwenyekiti wa maandalizi ya shuguli ya harambee ya wabunge, Profesa Anna Tibaijuka wakiwa tayari kusoma fedha wazilizo changisha wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akipokea hundi kutoka kwa wawakilishi wa benki ya NBC wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akipokea hundi kutoka kwa wawakilishi wa benki ya CRDB wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
*Spika mstaafu Makinda ashangazwa… atoa neno
*Dk.Tulia asema ili kufanikisha lengo zinahitaji Bil 3.5/-
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
CHAMA cha Wabunge Wanawake wa Bunge la Tanzania wamefanikiwa kukusanya Sh.milioni 800 kwenye harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo kitakachojengwa katika majimbo yote nchini.
Fedha hizo zimekusanywa jana kwenye harambee iliyofanyika Mliman City jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi kwenye harambee hiyo alikuwa Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda.
Tayari wabunge hao wanawake wamefanikiwa kukusanya jumla ya Sh.bilioni 2.5 kwani kabla ya harambee ya jana tayari walishafanya harambee nyingine ya kukusanya fedha jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa harambee hiyo Spika wa Bunge Job Ndugai amesema wanatambua umuhimu wa kuunga mkono jitihada za wabunge wanawake katika kuhakikisha wanatimiza lengo la ujenzi wa choo.
“Tumekutana hapa kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo.Lengo ni kujenga vyoo nchi nzima kwa maana ya majimbo yote,”amesema Ndugai.
Kwa upande wa mgeni rasmi Spika mstaafu wa Bunge Makinda amesema uamuzi ambao umefanywa na wabunge wanawake na kuungwa mkono na wabunge wanaume katika kufanikisha fedha zinapatikana ni wa kihistoria.
“Tunatambua changamoto ambazo wanafunzi wanazipata na hasa kwa mtoto wa kike kutokana na maumbile yake.Hivyo ujenzi wa choo cha mfano kitasaidia kuwafanya wanafunzi hao kufurahia mazingira yatakayokuwamo kwenye choo hicho.
“Tunafahamu binti wa kike anapovunja ungo akiwa shuleni kuna mabadiliko yanaanza kutokea na anapokuwa kwenye tarehe yake wengine wanatega shuleni kwa kuona hawako salama.Choo kitakachojengwa kitamfanya binti kutokuwa na wasiwasi hata akiwa kwenye tarehe za hedhi,”amefafanua.
Makinda ametoa ombi kwa Watanzania kokote walipo kuchangia ujenzi wa choo hicho kwani lengo na kumuondolea adha mwanafunzi na hasa mwanafunzi wa kike.
Pia amesema kitendo cha wabunge hao kuamua kuchangisha fedha kimemshangaza huku akiwaaambia wamefanya kitu kikubwa na chenye thamani.
Ameongeza mkombozi wa mtoto wa kike ni mazingia rafiki yanayomuwezesha kuwa huru kutimiza ndoto zake.
Wakati huo huo Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Akson amesema kuwa ili kufanikisha mchakato wa ujenzi wa vyoo hivyo zinahitajika Sh.bilioni 3.5 kwa nchi nzima.
Amesema wabunge wanawake wameona haja ya kuhakikisha wanakusanya fedha kwa ajili ya kujenga choo cha mfano kwa majimbo yote.
Amefafanua choo kimoja kitagharimu Sh.milioni 11 na hivyo ili kujenga kwenye majimbo yote wanahitaji Sh.bilioni 3.5.
Katika kufanikisha ukusanyaji huo wa fedha unafanikiwa taasisi, mashirika, kampuni binafsi, watu mashuhuri wabunge wameonesha mshikamano kwa kuchangia fedha hizo.
Pia ili kufanikisha harambee hiyo bidhaa mbalimbali zilipigwa mnada ambapo fedha zilizopatikana zinakwenda kwenye ujenzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: