Katikati ni Mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Pudensiana Mbwiliza akifungua bonanza la michezo kwa vijana kutoka halmashauri za wilaya mkoani Mwanza. Kushoto ni Mratibu wa Wahudumu wa jamii (HBC) kutoka halmashauri ya wilaya ya Misungwi Yahaya Isangula,kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akielezea lengo la bonanza la michezo.
Katikati ni Mwenyekiti wa Kikundi cha vijana cha 'Wise Youth' kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando, Douglas Renatus akitoa mwongozo wa kufanya michezo kwenye kundi lake wakati wa bonanza.
Kiongozi wa Kikundi cha vijana cha 'Wise Youth' kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando,Joan John akiongoza mchezo wa kabute.
Mchezo wa Chupa ukiendelea: Washiriki wa mchezo wakikimbizana na atakayewahi kukamata chupa ndiyo mshindi.
Mchezo wa kukamata limao kwa meno ndani ya ndoo ya maji kisha kushika chupa iliyopo katikati ukiendelea.
Mshindi wa mchezo wa kukamata limao kwa meno ndani ya maji akiwa na limao lake na chupa.
Mchezo wa kuruka ndoo: Kijana kafunikwa uso kisha kaambiwa kuwa kuna ndoo ya maji airuke.
Kijana akiruka juu akiamini kuwa kuna ndoo ya maji mbele yake.
Mbio za magunia nazo zilikuwepo.
Mbio za mita 100 zikiendelea.
Vijana wakishindana kunywa soda haraka.
Vijana kutoka halmashauri ya wilaya ya Sengerema wakionesha mchezo wa Vichekesho.
Vijana wakionesha igizo kuhusu umuhimu wa wana ndoa kupima VVU.
Picha ya pamoja washiriki wa bonanza.
Picha za vurugu washiriki wa bonanza la michezo.
Picha ya pamoja Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Pudensiana Mbwiliza na walezi wa vijana mkoani Mwanza.
Kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akimpa zawadi ya maua Pudensiana Mbwiliza ikiwa ni sehemu ya pongezi kwake kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania hivi karibuni.
Cecilia na Douglas wakimpa zawadi ya maua Pudensiana.
Pundensiana akiwa na maua yake.
Vijana mkoani Mwanza wamelishukuru Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kuwa karibu na vijana wanaopata huduma kwenye vituo vya tiba na matunzo.
Wakizungumza jana Septemba 8,2018 wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika katika Viwanja vya Lessa Garden Hotel jijini Mwanza,vijana hao walisema shirika la AGPAHI limekuwa msaada mkubwa kwa vijana kwani mbali na kutoa huduma kwenye vituo vya tiba na matunzo pia limekuwa likiandaa michezo kwa vijana.
Aidha walisema lengo la bonanza hilo lililokutanisha vijana wanaotoka katika klabu za vijana zilizoundwa na zinasimamiwa na AGPAHI katika halmashauri mbalimbali ni kwa ajili ya vijana kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki wapya,kuonyesha vipaji na kujifunza.
Akifungua bonanza hilo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Pudensiana Mbwiliza aliwataka vijana kutokata tamaa katika maisha huku akiwasititiza kuwa wamoja na kuendelea kushirikiana.
“Nawaomba vijana ambao wamepata maambukizi ya VVU kuendelea kuwa wafuasi wazuri wa dawa za kufubaza makali ya VVU ARVs,kwani kupata maambukizi haimaanishi ndiyo mwisho wa maisha”,alisema Mbwiliza.
Naye Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona alisema vijana walioshiriki katika bonanza ambalo limefadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC) wanatoka katika halmashauri za wilaya za Misungwi,Sengerema,Nyamagana,Magu na Kwimba.
Alitumia fursa hiyo kuwasihi vijana kutafakari kwa makini kabla ya kufanya maamuzi katika maisha na kuepuka kupoteza mwelekeo kutokana na maneno ya watu wanaowazunguka katika jamii.
Miongoni mwa michezo iliyofanyika katika bonanza ni kukimbia mita 100,mbio za magunia,kushindana kunywa soda,mchezo wa chupa,kukimbia na malimao na mayai,kabute,kuruka ndoo,kukamata limao kwenye maji kwa meno,maigizo na vichekesho.
Toa Maoni Yako:
0 comments: